Nenda kwa yaliyomo

Edgar Ngelela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Edgar Ngelela

Maelezo ya awali
Amezaliwa 15 Oktoba 1980 (1980-10-15) (umri 44)
Kazi yake Mwimbaji, Mtunzi, Muigizaji, Muongozaji na mtengeneza Filamu

Edgar Leonard Luhende Ngelela (amezaliwa Morogoro, Tanzania, 15 Oktoba 1980[1]) ni msanii katika masuala ya muziki, uchoraji, uigizaji, uongozaji wa michezo ya jukwaa na ya runinga na utengenezaji wa filamu kutoka nchini Tanzania. Ikiwa na pamoja na kucheza maigizo bubu, muziki, kuchora, kubuni na kutengeneza filamu ametumia elimu yake katika kufundisha sehemu mbalimbali kama Chuo kikuu cha Dar es Salaam na TFTC.

Mwaka 2013 Ngelela alitengeneza filamu fupi iitwayo 'Anguko' ambayo ilishiriki katika matamasha mbalimbali ya filamu. Haya ni pamoja na Tamasha la majahazi Zanzibar, Archived 21 Machi 2019 at the Wayback Machine. (The Zanzibar International film festival; ZIFF) Archived 21 Machi 2019 at the Wayback Machine.,na Arusha Afirican film festival (AAFF) Archived 17 Oktoba 2013 at the Wayback Machine..

Edgar Ngelela, 2012

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Edgar Ngelela alizaliwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Akiwa mtoto wa hayati Felix Ngelela Luhende na mama Hildegald Lyimo Luhende, wazazi wake walihamia Mkoani Shinyanga akiwa bado mdogo. Huko walizaliwa wadogo zake: Nicholaus Ngelela Luhende na Benedict Ngelela (Bennysofar).

Alianza kusoma elimu ya awali maarufu kama vidudu, kabla ya kuanza darasa la kwanza mwaka 1987 katika shule ya msingi Mwenge, lakini mwaka huohuo alihamia katika shule ya kimataifa iliyoko mkoani Arusha inayoitwa Mtakatifu Constantine, ambako aliendelea hadi darasa la tatu, na baadaye kutokana na hali ya hewa mkoani humo, ilimshinda Edgar kiafya. Hivyo, familia yake iliamua kumwamishia katika shule ya msingi ya Nyakahoja iliyoko mkoani Mwanza, ambapo ndipo alipomalizia elimu yake ya msingi.

Baada ya kumaliza darasa la saba, aliendelea na masomo yake ya sekondari ya awali katika shule ya Lububu katika wilaya ya Nzega Mkoani Tabora, ambapo alisoma kwa muda wa miezi minne kutokana na sababu mbalimbali hakuweza kuendelea na masomo kwani alisoma miezi minne tu, kati ya miezi kumi na mbili aliyotakiwa kusoma.

Mwaka uliofutia, yaani mwaka 1996, alihamishiwa nchini Kenya ambapo kutokana na utaratibu wa elimu ya nchini Kenya alitakiwa kufanya maandalizi kabla ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa muda wa mwaka mmoja na mwaka 1997, alianza kidato cha kwanza katika shule ya wavulana ya Isebania iliyoko kama kilometa mbili kutoka katika mpaka wa Sirari katika wilaya ya Kurya hadi mwaka 2000, ambapo alimaliza kidato cha nne katika shule hiyo.

Katika sanaa Ngelela alionekana kuwa na kipaji kikubwa jambo ambalo lilichangia kupata ruhusa kwa wazazi wake kwenda kusomea sanaa katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) ambapo alichukuwa stashahada yake ya sanaa. Baadaye Ngelela alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo alichukua Shahada yake ya kwanza na shahada ya uzamili ya sanaa za maonesho na sanaa za ufundi.

Huku akiwa anatuma maombi katika vyuo mbalimbali hatimaye alipata nafasi katika chuo cha sanaa Bagamoyo nchini Tanzania ambapo alikuwa akichukua stashahada ya sanaa kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kuhitimu masomo yake ya sanaa chuoni hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alikuwa akichukua shahada ya Sanaa ya Maonesho na Sanaa ya Ufundi (Bachelor of Arts in Fine and Performing Arts) ambapo mwaka 2008, alitunukiwa shahada yake ya kwanza katika masuala ya sanaa za maonesho na sanaa za ufundi.

Baada ya kumaliza elimu yake katika chuo kuku cha Dar es Salaam na kupata shahada yake, alianza kuchua shahada ya uzamili katika masuala hayo hayo ya sanaa, masomo aliyohitimu mwaka 2010.

Bagamoyo

[hariri | hariri chanzo]

Edgar alianza kusoma masomo yake ya sanaa katika chuo cha sanaa Bagamoyo mwaka 2001, akiwa na wimbo wake mmoja alioutunga tangu akiwa shule ya sekondari, lakini akiwa chuoni hapo, Edgar alipata wazo la kutunga wimbo wake mwingine katika lugha ya Kiswahili ambapo mwaka huo huo alitunga wimbo wake wa Kiswahili uliojulikana kama Mpweke kutokana na kuwa mpweke katika sanaa kutokana na familia yake kushindwa kumkubali kama msanii.

Upigaji gitaa

[hariri | hariri chanzo]

Mwezi wa kumi mwaka 2001, Edgar alianza rasmi mafunzo ya kupiga gitaa, na hadi kufikia mwezi wa kumi na mbili akiwa tayari ameshatunga wimbo wake wa mpweke alianza kutunga na kuimba kwa kutumia gitaa, ambapo alikuwa bado akiimba kama msanii mdogo.

Akiwa hapo chuoni, alipata nafasi ya kukutana na wasanii wakongwe kama vile, Vitalis Maembe, ambaye ni msanii aliye rekodi nyimbo nyingi za asili, John Sombi ambaye naye ni msanii katika nyimbo za asili na amesharekodi nyimbo mbalimbali.

Chuo cha Bagamoyo kiliamua kutunga nyimbo mbalimbali katika album ambapo Edgar alishiriki kama mpiga gitaa katika nyimbo mbalimbali kama vile , Sumu ya teja, na masamva za wasanii wa Bagamoyo. Huku akiwa ndio anamalizia mwaka wake wa kwanza.

Baada ya Bagamoyo

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kumaliza chuo cha sanaa Bagamo, Edgar alirudi nyumbani na baadae kidogo alipata nafasi ya kwenda kufanya onesho nchini Uingereza katika sanaa ya maigizo na nyimbo, katika eneo la North Landon ukumbi Azure karibu na uwanja wa Wimbley. Baada ya kurudi kutoka Uingereza, Edgar alipata nafasi ya kurekodi wimbo wake wa kwanza katika studio ya Zamunda na ndio aliporekodi wimbio wa Sema Ndio, hii ikiwa ni mwaka 2005. wimbo ambao bado haukumaliziwa na kuachwa kama demo. Hii ilitokana na ushauri wa mtayarishaji wa nyimbo hiyo kuwa ibaki studio kwa muda kidogo ikisubiria wakati wake.

Baadae alianza masomo ya chuo kikuu, na mwaka 2006, alikutana rafiki yake anayeitwa Edson Tibaijuka na kuanzisha kundi linaloitwa E2E ambapo lilidumu kwa muda wa mwaka mzima, ambapo Edson aliliimarisha Kundi lake la awali la Da'voice na kwa kushirikiana na Edgar na kufanya kundi la watu hilo kuwa na watu wanne. Huku Edgar akiwa na ujuzi wa kupiga gitaa, aliendelea kupiga gitaa katika nyimbo mbalimbali.

Kabla ya kuamua kurekodi nyimbo zake, walirekodi wimbo akiwa na kundi la Da'voices, na kurekodi nyimbo kama 'Promise' na 'Inaniuma' ambazo katika nyimbo hizo Edgar alipiga gitaa.

Mwaka 2009, mwezi wa kumi, ndipo walipoanza kutafuta kurekodi wimbo wao wenyewe kama kundi la Dar Voices, ambao wamaeshirikina na msanii mweingine anaitwa Chiss Mc, katika wimbo naona ambao Edgar aliimba na kupiga gitaa. Mpaka sasa kama Da'voice wamerekodi nyimbo mbalimbali.

Edgar alianza kufanya sanaa tangu akiwa mdogo sana, kabla hata hajaanza kusoma shule yoyote, lakini baada ya kuanza shule ya msingi, Edgar aliendelea na shughuli za Uchoraji pamoja na muziki huku akiwa ansoma, jambo ammbalo familia yake haikulipenda kwa kuhisi kuwa alikuwa hatumii muda wake kusoma.

Akiwa shuleni katika shule ya Msingi Nyakahoja akiwa darasa la nne alianza kuigiza na hapo ndipo walianza kumpenda na kumpa nafasi mbalimbali za kuingiza hasa uigizaji mkuu kutokana na kuonekana kuwa na kipaji cha sanaa. Alipomaliza elimu yake ya msingi, Edgar alizawadiwa cheti cha uchoraji, miziki na uigizaji, kutokana kuonesha kuwa na kipaji

Baada ya kumaliza elimu ya msingi, Edgar hakuishia hapo kwani alipoanza kidato cha kwanza katika sekondari ya Isebabia nchini Kenya alichaguliwa kuwa kiongozi katika maswala ya Burudani mbalimbali, na pia alikuwa mwenyekiti wa Klabu za sanaa mbalimbali hapo shuleni. Wakati akiwa binafsi anaendelea kuimba na kuchora. Mara nyingi alikuwa akiimba nyimbo za wanamuziki wengine.

Baada ya kufika kidato cha pili, Edgar aliamua kutunga wimbo wake mwenyewe wa kwanza ambao ulikuwa katika lugha ya kiingerwza ulioitwa so many reasons, ambao haukupata nafasi ya kurekodiwa na badala yake alikuwa akiimba katika matamasha mbalimbali ya kishule. Ngelela alianza kuigiza akiwa mdogo sana. Kipaji chake kilionekana zaidi akiwa shule ya msingi. Hakuishia hapo, kipaji chake kilijitokeza zaidi tena akiwa bagamogo pale alipoonekana kuwa mmoja wa waigizaji wazuri wa maigizo bubu (Mime). Mwaka 2005 yeye na mwenzie aitwaye Catherine Mponda ambao wote walifanya vizuri sana katika masomo yao ya sanaa walipata nafasi ya kushirikiana na waalimu watano wa TaSUBa kwenda Uingereza (London) kufanya onesho la jukwaa lililojulikana kwa jina la 'Umoja' katika jumba la Azure lililoko jirani na uwanja wa Wembley ulioko uingereza kaskazini (North London).

Muziki umekuwa moja ya sanaa ambazo Edgar Ngelela amekuwa akizipenda. Alianza kwa kuimba katika miaka yake ya shule ya msingi lakini kwa muda mrefu alikuwa akiimba nyimbo za watu. Mwaka 1999 aliandika nyimbo yake ya kwanza iliyoitwa 'Sababu nyingi' (So many reasons) lakini pamoja na nyimbo mbili zilizofuatia hakuwahi kuzirekodi. Mwaka 2001 akiwa TaSUBa alitunga wimbo wake wa kwanza wa kiswahili uliyoitwa 'Mpweke'. Hapa aliongeza juhudi katika kujifunza upigaji wa gitaa. Muda si mrefu alifanikiwa kuimba na kuzipiga nyimbo zake kwenye gitaa. Kwa nafasi aliyokuwa nayo TaSUBa Ngelela alipata nafasi ya kukutana na wasanii wakongwe kama Vitalis Maembe; msanii aliyerekodi nyimbo nyingi zenye mahadhi ya kiasili na zenye ujumbe mzito. Ngelela ameshirikishwa na Vitalis Maembe kama mpiga solo gitaa kwenye wimbo wa Sumu ya teja na mpiga bass gitaa kwenye wimbo wa John Sombi ulioitwa Masamva.

Mwaka 2005 akiwa amemaliza TaSUBa Ngelela alirekodi wimbo wake wa kwanza ulioitwa Sema ndiyo ambao haukumaliziwa kufanyika kutokana na matatizo ya kiufundi. Mwaka 2006 akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikutana rafiki yake anayeitwa Edson Tibaijuka na kuanzisha kundi la E2E. Mwaka mmoja baadaye kundi lilibadili jina na kuitwa Da'voice jina ambalo lilikuwa na historia yake. Likiwa na watu watatu yaani pamoja na Seki B Edgar mwaka 2008 walifanikiwa kurekodi nyimbo nyingi kama Promise, Mpweke na Take you tonight

Sanaa nyingine

[hariri | hariri chanzo]

Zaidi ya Uigizaji, Uongozaji na muziki Ngelela pia ni mchoraji, mhariri wa picha na mpiga picha wa filamu na video.

Uchoraji

[hariri | hariri chanzo]

Edgar kwa sasa anatengeneza kitabu cha katuni kinachoitwa Marcus, ambapo kinahusisha hadithi za katuni, pia ametafsiri kitabu cha Muheshimiwa mstahiki bwana Maneno ambapo hadi hivi sasa bado anashughulika na wataalamu mbalimbali wa michezo ya kuigiza kama vile Bwana Edwin Semzaba ili kuusahihisha kama mchezo wa kuigiza.

Uigizaji

[hariri | hariri chanzo]

Katika sanaa za waigizaji naye ni miongoni mwa watu wachacha katika Tanzania wenye uwezo wa kufanya maigizo bubu (mime), na amefundishwa na Bwana Nkwabi Nhangasamala aliyepata ujuzi huo nchini Ujerumani.

Sanaa ya picha

[hariri | hariri chanzo]

Akiwa kidato cha tatu Kaka yake Edgar alirudi kutoka Urusi akiwa na kifaa cha kupigia picha au kamera na kumpa Edgar ambapo ndipo Edgar alipovutiwa masuala ya kupiga picha na kuanza kujifunza kupiga picha huku akipiga picha katika sherehe mbalimbali.

Kazi za kujitegemea

[hariri | hariri chanzo]

Anatarajia Kutengeneza nyimbo za kutosha katika aina mbalimbali za tamaduni, zinazojulikana kama mix culture , na kutoa nyimbo mbalimbali, mazingira ya nyimbo ambazo zimechanganya tamaduni mbalimbali na kushirikiana na wasanii mbalimbali.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • So many reasons- 2001
  • Mpweke - 2001
  • Sumu ya teja- 2001
  • Inaniuma 2009

Tofauti na nyimbo, Edgar pia anatarajia kutengeza picha katika nyimbo mbalimbali huku akiwa tayari ameshatengezeza video katika nyimbo mbalimbali.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Tovuti rasmi ya Edgar Ngelela

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edgar Ngelela kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.