Nenda kwa yaliyomo

Eazy-E

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eazy-E
Eazy-E mnamo 1993
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaEric Lynn Wright
Amezaliwa(1964-09-07)Septemba 7, 1964
Compton, California, U.S.
Amekufa26 Machi 1995 (umri 30)
Los Angeles, California, U.S.
Kazi yakeRapper, CEO, mtayarishaji wa rekodi
Miaka ya kazi1986–1995
StudioRuthless, Priority, Relativity, Epic, MCA
Ameshirikiana naN.W.A, DJ Yella, Dr. Dre, The D.O.C., Rhythum D, Above the Law, B.G. Knocc Out & Dresta, Bone Thugs-n-Harmony, Sylk-E. Fyne, Ice Cube, Brownside

Eric Lynn Wright (7 Septemba 196426 Machi 1995) alikuwa rapa na mtayarishaji wa muziki kutoka mjini Compton, California, Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Eazy-E. Wakati Eazy E bado yungali bwana mdogo alikuwa akijishughulisha na maswala ya uuzaji wa dawa za kulevya, kisha pesa za kazi hiyo anawekeza katika mradi wake wa muziki wa hip hop.

Anafikirika sana kuwa yeye ni mmoja kati ya waanzilishi wakubwa wa kundi la muziki wa hip hip maarufu kama N.W.A., lakini baadaye alipata umaarufu zaidi pale alipokuwa akifanya muziki huo akiwa kama msanii wa kujitegemea (solo artist).

Sauti ya Eazy-E ilikuwa ikijulikana kwakuwa alikuwa akiitumia kwa staili moja tu, alikuwa akiimba kwa sauti ya juu na mashairi yake yalikuwa yakilenga sana maisha ya mtaani, yaani ujambazi, madawa ya kulevya, mahusiano ya wakazi na polisi, na masuala ya kujamiiana.

Kuna kipindi pia alikuwa akitangaza kipindi cha hip hop katika radio ya Los Angeles katika kituo cha KKBT.[1]

Kwa kazi zake za uuzaji wa dawa za kulevya, zilikuwa zikimpa faida sana na akaamua kutumia faida zake kwa kuanzisha studio ya kurekodia mzuiki huo. Studio ilikwenda kwa jina la Ruthless Records.[1] Pale Ruthless ilipo msajiri Dr. Dre na Ice Cube wakatunga nyimbo ya "Boyz-n-the-Hood", kisha Wright akaanzisha kundi liliokwenda kwa jina la N.W.A, kundi likaunganisha marapa wengi kama Dr. Dre na Ice Cube kisha baadaye akaongezeka DJ Yella na Arabian Prince. Baadaye studio ya Ruthless ikatoa albamu ya kwanza ya N.W.A (1987), N.W.A na mwaka uliofuata wakatoa Straight Outta Compton (1988), na baada ya mwezi mmoja Eazy-E akatoa albamu yake binafsi iliyokwenda kwa jina la Eazy-Duz-It.

Albamu za Easy-E[hariri | hariri chanzo]

  • 1988: Eazy-Duz-It
  • 1992: 5150: Home 4 tha Sick
  • 1993: It's On (Dr. Dre) 187um Killa
  • 1995: Str8 off tha Streetz of Muthaphukkin Compton
  • 1996: Eternal E
  • 2002: Impact of a Legend
  • 2007: Featuring…Eazy-E

Marejeo ya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Pareles, Jon. "Eazy-E, 31, Performer Who Put Gangster Rap on the Charts", The New York Times, 1995-03-28. Retrieved on 2008-03-08. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]