Dusan Tadic

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tadic mwaka 2018
Dusan Tadic

Dušan Tadić (kwa Kiserbia: Душан Тадић dushan taditsh; alizaliwa 20 Novemba 1988) ni mchezaji wa soka wa Serbia ambaye anacheza klabu ya Uholanzi ya Ajax na timu ya taifa ya Serbia.

Alitumia ujana wake katika klabu ya AIK Bačka Topola na FK Vojvodina, hatimaye kucheza katika UEFA (ligi kuu ya Ulaya). Baada ya misimu miwili na FC Groningen nchini Uholanzi alijiunga na FC Twente mwaka 2012, ambapo alipata fursa ya kujiunga na klabu ya Southampton ya Ligi Kuu Uingereza. Baada ya miaka minne huko Uingereza, Tadić alirudi Uholanzi mwaka 2018, alipojiunga na Ajax.

Tadić amecheza zaidi ya mechi 60 kwa Serbia, baada ya kuanza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwaka 2008, na kuiwakilisha nchi katika Olimpiki mwaka huo, pamoja na Kombe la Dunia la FIFA 2018.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dusan Tadic kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.