Doto Mashaka Biteko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Doto Mashaka Biteko (amezaliwa 30 Desemba 1978) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Bukombe kwa awamu mbili, mwaka 20152020 na 2020-2025. [1] Alipata elimu ya msingi kuanzia mwaka 1988 hadi 1994 Shule ya msingi Nyaruyeye kabla ya kujiunga na shule ya Sekondari Sengerema kuanzia mwaka 1995 hadi 1998. Alipata Cheti cha ualimu daraja la IIIA katika chuo cha Ualimu Katoke kilichopo Wilaya Muleba mkoani Kagera kuanzia mwaka 1999 hadi 2001, baadae alijiunga na Chuo cha ualimu Butimba mkoani Mwanza ambapo alisomea Theater art na kupata cheti kati ya mwaka 2002 hadi 2004. Mwaka 2005 hadi 2007 alijiunga na Chuo cha ualimu Morogoro na kuhitimu Stashahada, alijiunga na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine na kupata shahda ya awali katika ualimu kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 na baadae kupata shahada ya uzamili mwaka 2011 hadi 2013.[2]

Aliteuliwa kuwa naibu waziri wa Madini mwaka 2017 kabla ya kuteuliwa kuwa waziri wa madini wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2019. August 2023 ameteuliwa kuwa naibu Waziri Mkuu (mratibu wa shughuli za Serikali) na waziri wa Nishati katika Mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu yaliyotolewa tarehe 30 Agusti 2023. [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  2. Tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliangaliwa Septemba 03, 2023.
  3. [https://www.ikulu.go.tz Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tovuti Rasmi ya Rais], iliangaliwa Septemba 03, 2023.