Dola (pesa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Dola 20 za Marekani

Dolar (pia dola, Kiing. dollar) ni jina la pesa ya Marekani na nchi mbalimbali duniani. Dola ya Marekani au US-Dollar inajulikana zaidi, lakini kuna nchi zaidi za 20 zinazotumia neno "Dollar" kwa pesa yao.

Nchi zenye pesa inayoitwa "Dollar" (dola)[hariri | hariri chanzo]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Asili ya jina hili ni neno la Kijerumani "taler" (au: thaler) kwa ajili ya sarafu ya fedha iliyotolewa kwenye mji wa Joachimsthal kule Bohemia mnamo mwaka 1518. Wakati ule migodi ya Joachimsthal ilikuwa na fedha nyingi kiasi cha kwamba mji ulianza kutoa pesa yake. Pesa hizi zilitwa kufuatana na mji "Joachimsthaler" iliyofupishwa kuwa "taler" tu. Taler ilikuwa peda iliyopendwa sana Ulaya ikasambaa kote. Hispania ilitumia jina hili kwa "dolaro" yake kuanzia 1575. Dolaro hii ya Hispania ilikuwa baadaye pesa ya kisheria ya Marekani ilipojitenga na Uingereza na kuanzisha pesa yake 1792.