Nenda kwa yaliyomo

Dexta Daps

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Louis Anthony Grandison (anajulikana kwa jina lake la kisanii Dexta Daps, Dappa Don au Dexta, alizaliwa 12 Januari 1986) ni mtumbuizaji wa dancehall na reggae kutoka Jamaika.

Kazi ya Grandison ilianza mwaka 2012 na kutoa nyimbo zake mbili za kwanza "Save me Jah" na "May You Be".[1] Ingawa ametoa nyimbo nyingi kati ya vipindi hivyo (kama vile "Grease mi Gun" na "Dis a Di Bess"), alianza kupata kutambulika sana kwa umma mwaka 2014 kupitia nyimbo zake "Morning Love" na "Jealous Ova", ambapo ya mwisho ilimshirikisha msanii mwingine chipukizi wa dancehall, Tifa.[2] Dexta Daps aliendeleza umaarufu wake hadi mwaka 2015. Wimbo wake "Shabba Madda Pot" ulipata zaidi ya watazamaji milioni 13 kwenye YouTube na huu ni mmoja wa nyimbo maarufu zaidi za Grandison. Amefanya ushirikiano na wasanii wengi wa dancehall kama Kranium, Masicka, Movado na wasanii wa kimataifa kama M.I.A, Davido, Kiesza na Tory Lanez. Dexta Daps anasifiwa kwa uhodari wake, sauti yake ya kipekee, mtindo wake na maonyesho yake.[3]

  1. reggaeville. "Biography: Dexta Daps". www.reggaeville.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-11-30.
  2. "Tifa Biography, Songs, & Albums". AllMusic (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-11-30.
  3. reggaeville. "Biography: Dexta Daps". www.reggaeville.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-11-30.