Dennis Kipruto Kimetto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dennis Kipruto Kimetto (alizaliwa 22 Januari 1984) ni mwanariadha wa masafa mrefu wa Kenya ambaye hukimbia katika mashindano ya kukimbia barabarani. Kimetto alikuwa na rekodi ya ulimwengu kwa marathoni ya wanaume na wakati ya 2:02:57. Yeye alikuwa na rekodi hiyo mpaka Eliud Kipchoge alipovunja rekodi mwaka wa 2018.

Dennis Kipruto Kimetto
Sport
CountryKenya Kenya
SportRiadha
Event(s)mbio za masafa marefu

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kimetto anatoka mji wa Eldoret. Yeye alikulia kijijini katika mkoa wa bonde la ufa. “Nadhani kinachonitia motisha kuwa mpiganaji ni ukweli kwamba ninatoka katika hali ngumu. Ninajaribu kuhakikisha kuwa ninatimiza bora yangu ili niweze kusaidia familia yangu”.

Alikuwa mwanachama wa kikundi cha mafunzo kilichoongozwa na Geoffrey Mutai. Kimetto alipata ushindi mkubwa wa kwanza katika nusu marathoni wakati wa marathoni ya Nairobi mwaka 2011. Yeye alishinda na wakati ya 1:01:30.

Kimetto alipata umaarufu aliposhindana nje ya Kenya. Kimetto aliposhinda Nusu Marathon ya Berlin, umri wake uliripotiwa vibaya na watu walisema kwamba Kimetto ana miaka kumi pungufu kuliko alivyosema. Kwa hiyo watu walifikiri kwamba Kimetto alikuwa na rekodi ya ulimwengu ya vijana. Jina lake liliripotiwa kama Dennis Koech pia. Sababu ya yote hayo ilikuwa ni makosa kwenye pasipoti yake. Hii ilirekebishwa katika mashindano ya baadaye.

Kimetto aliendelea hadi kuvunja rekodi katika BIG 25 Berlin. Baadaye yeye alishindana na alikimbia kasi zaidi ya yeyote katika historia katika marathon ya kwanza yake. Tena huko Berlin, Kimetto alikimbia na Geoffery Mutai kwa sehemu kubwa ya mashindano na alimaliza sekunde moja nyuma ya Mutai na alikuwa na nafasi ya tano wenye kasi zaidi kuwahi kukimbia wakati huo. Baadhi ya waandishi wa habari walisema kwamba Kimetto alikaa nyuma ya Mutai wakati wa sehemu wa mwisho ya mashindano kwa sababu yeye alimtakia Mutai kupata Kombe la safu ya Marathon ya Ulimwengu ya watu wazima.

Mwaka 2013 Kimetto alivunja rekodi mbili katika kozi mbili katika Marathon ya Ulimwengu ya watu wazima. Alivunja rekodi katika mji wa Tokyo na wakati wa 2:06:50 na alivunja rekodi tena katika mji wa Chicago na wakati wa 2:03:45, wakati bora kabisa katika kozi ya ubora wa rekodi Marekani wakati huo. Mwaka 2014 mwezi wa tisa siku ya ishirini na nane, Kimetto alivunja rekodi ya ulimwengu katika Berlin Marathon na wakati wa 2:02:57 na akakuwa mwanaume wa kwanza alikimbia chini ya wakati 2:03. Isipokuwa wakati ya kuteremka na kusaidiwa sana na upepo katika Marathon ya Boston nusu wapili wa mbio yake ilikuwa haraka sana katika historia. Mwaka 2015 majira yake yalikuwa sio mazuri kama majira yaliopita kwa sababu yeye alimaliza tu Marathon ya London katika nafasi ya tatu. Kimetto hakumaliza IAAF Marathon ya Mashindano ya Dunia katika Beijing au Marathon ya Fukuoka kwa sababu alipata jeraha. Jeraha hili lilimfanya akose Olimpiki ya Rio na Marathon ya Chicago pia. Shinda za kuumia za Kimetto ziliendelea mwaka 2017, na jeraha la goti lilimfanya akose Marathon ya Boston. Kimetto hakuweza kumaliza Marathon ya Honolulu na Marathon ya Chicago tena mwaka huo huo.

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

  • Matokeo yote kuhusu marathoni na nusu marathoni
Bendera ya Kenya Kenya
2011 Nairobi Half Marathon Nairobi, Kenya 1st 1:01:30
RAK Half Marathon Dubai, United Arab Emirates 1st 1:00:40
2012 Berlin Half Marathon Berlin, Germany 1st 59:14
BIG 25 Berlin Berlin, Germany 1st 1:11:18
Berlin Marathon Berlin, Germany 2nd 2:04:16
2013 Tokyo Marathon Tokyo, Japan 1st 2:06:50
Chicago Marathon Chicago, United States 1st 2:03:45
2014 Berlin Marathon Berlin, Germany 1st 2:02:57 (WR)
2015 London Marathon London, England 3rd 2:05:50
2016 London Marathon London, England 9th 2:11:44
2018 Shanghai International Marathon Shanghai, China 10th 2:14:54
Ratiba ya matokeo ya Mashindano ya Dunia ya Marathoni
Mashindano ya Dunia ya Marathoni 2012 2013 2014 2015 2016
Tokyo Marathon - 1st - - -
Boston Marathon - - - - -
London Marathon - - - 3rd 9th
Berlin Marathon 2nd - 1st - -
Chicago Marathon - 1st - - -
New York City Marathon - - - - -

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]