Nenda kwa yaliyomo

Dennis Hopper

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dennis Hopper

Hopper mnamo Machi Kigezo:2010, miezi miwili kabla ya kufa kwake
Amezaliwa Dennis Lee Hopper
(1936-05-17)Mei 17, 1936
Dodge City, Kansas, U.S.
Amekufa Mei 29, 2010 (umri 74)
Kazi yake Mwigizaji, mwongozaji, msanii
Miaka ya kazi Kigezo:1955–2010
Ndoa Brooke Hayward (1961–1969)
Michelle Phillips (1970)
Daria Halprin (1972–1976)
Katherine LaNasa (1989–1992)
Victoria Duffy (1996–2010)

Dennis Lee Hopper (17 Mei 1936 - 29 Mei 2010) alikuwa mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, na msanii kutoka nchini Marekani. Akiwa bwana mdogo, Hopper akawa na shauku ya uigizaji na hatimaye akawa mwanafunzi wa Actors Studio. Amefanya onekano lake la kwanza katika televisheini mnamo mwaka wa {1955}, ana akaonekana kwenye filamu mbili akiwa na James Dean, Rebel Without a Cause (1955) na Giant (1956). Miaka kumi iliyofuata, Hopper akaonekana mara kwa mara kwenye michezo ya televisheni akicheza nyusika za ugeni, na kufikiwa mwishoni mwa miaka ya [1960] amecheza kama mwigizaji msaidizi kwenye filamu mbalimbali.

Amepata kuongoza na kuigiza kwenye filamu ya Easy Rider (1969), akishinda tuzo kwenye Cannes Film Festival na akachaguliwa kwenye Academy Award kwa ajili ya Best Original Screenplay akiwa kama mwandishi-mshirika. Mtahakiki wa filamu Matthew Hays alieleza kwamba "hakuna mtu mwingine anayekubalika sana kwa kuonyesha kanuni za maisha fulani yalipotea ya miaka ya 1960 zaidi ya Dennis Hopper."[1]

Hakuwa na uwezo wa kujenga mafanikio yake mwenyewe kwa miaka kadhaa, hadi hapo alipokuja kushirikishwa kwenye Apocalypse Now (1979) imemleta mwamko. Baadaye akaja-kuonekana kwenye Rumble Fish (1983) na The Osterman Weekend (1983), na akapata umaarufu mkubwa sana kwa ajili ya kazi yake kwenye Blue Velvet na Hoosiers, na kwa kazi zake za baadaye zilimsukuma na kupata kuchaguliwa kwenye Academy Award kwa ajili ya Best Supporting Actor. Ameongoza filamu ya Colors (1988). Hopper kwenye filamu ya mwaka wa 1989 "Flashback" ambayo ilitokana na Love Movement ya miaka ya 1960. Pia amepata kucheza kama adui kwenye filamu ya Speed (1994) na Waterworld (1995). Kazi za Hopper za baaaye ni pamoja na uhusika mkuu wa mfululizo wa televisheni, Crash.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Hopper alizaliwa mjini Dodge City, Kansas, akiwa kama mtoto wa Marjorie Mae (amekufa 2006),[2] na Jay Millard Hopper[3] (Juni 1916 – Agosti[4] 1982).

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, familia yake ikahamia mjini Kansas City, Missouri, ambapo bwana mdogo Hopper alihitimu masomo ya sanaa ya kila Jumamosi katika Kansas City Art Institute, alifundishwa na Thomas Hart Benton. Akiwa na umri wa miaka 13, Hopper na familia yake wakahamia San Diego, ambapo mama'ke alifanya kazi kama mwelekezaji wa uokoaji wa majini na baba'ke alikuwa meneja wa kituo cha polisi (Hopper alitambua, lakini, kwamba baba'ke alikuwa kwenye ofisi za OSS, mjumbe wa CIA).[5] Hopper alipigiwa kura kwa kuigiza vizuri wakati anasoma elimu ya juu (Helix High School, La Mesa, California, kitongoji cha San Diego). Hapo ndipo alipopata shauku ya kujiendeleza katika masuala ya uigizaji, alisoma katika chuo cha Old Globe Theatre cha mjini San Diego, na Actors Studio ya mjini New York City (alisoma na Lee Strasberg kwa takriban miaka mitano). Hopper akapenda urafiki na mwigizaji Vincent Price, ambaye anapenda sana mambo ya sanaa na kumvutia Hopper kufanya sanaa. Alipenda sana michezo ya William Shakespeare.

Shughuli za filamu

[hariri | hariri chanzo]

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]

Alizoshiriki

[hariri | hariri chanzo]


  • Biskind, Peter. Easy Riders, Raging Bulls: How the Sex-Drugs-and-Rock 'N' Roll Generation Saved Hollywood, Simon and Schuster (1999)
  • Hoberman, J. Dennis Hopper: From Method to Madness, Walker Art Center (1988)
  • Hopper, Dennis. Dennis Hopper: Out of the Sixties, Twelvetrees Press (1986)
  • Rodriguez, Elean. Dennis Hopper: A Madness to his Method, St. Martin's Press (1988)

Makala za Hopper

[hariri | hariri chanzo]
  • "Dennis Hopper, Riding High," Playboy (Chicago), Dec. 1969
  • Interview with G. O'Brien and M. Netter, in Inter/View (New York), Feb. 1972
  • Interview in Cahiers du Cinema (Paris), Julai-Agosti 1980
  • "How Far to the Last Movie?," Monthly Film Bulleting (London) Oct. 1982
  • "Citizen Hopper," interview with C. Hodenfield, in Film Comment (New York) Nov/Dec. Kigezo:1986
  • Interview with B. Kelly, in American Film (Los Angeles) Machi 1988
  • Interview with David Denicolo, in Interview (New York), Feb. 1990
  • "Sean Penn," interview with Julian Schnabel and Dennis Hopper, Interview (New York) Sept. 1991
  • "Gary Oldman," in Interview (New York), Jan. 1992

Makala kuhusu Hopper

[hariri | hariri chanzo]
  • Macklin, F. A., "Easy Rider: The Initiation of Dennis Hopper," in Film Heritage (Dayton, Ohio), Fall 1969
  • Burke, Tom, "Dennis Hopper Saves the Movies," in Esquire (New York), Dec. 1970
  • Burns, Dan E., "Dennis Hopper's The Last Movie: Beginning of the End,", in Literature/Film Quarterly,1979
  • Algar, N., "Hopper at Birmingham," in Sight and Sound (London), Summer 1982
  • Herring, H. D., "Out f the Dream and into the Nightmare: Dennis Hopper's Apocalyptic Vision of America," in Journal of Popular Film (Washington, D.C.), Winter 1983
  • Scharres, B., "From Out of the Blue: The Return of Dennis Hopper," in Journal of the University Film and Video Assoc. (Carbondale, IL), Spring 1983
  • Current Biography 1987, New York, 1987
  • Martin, A., "Dennis Hopper: Out of the Blue and into the Black," in Cinema Papers (Melbourne), Julai 1987
  • Weber, Bruce, "A Wild Man is Mellowing, Albeit Not on Screen," in New York Times, Sept. 8, 1994


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  1. Unterburger, Amy L. (editor) International Dictionary of Films and Filmmakers - vol 3 Actors and Actresses, St. James Press (1997) p. 564
  2. Staff (11 Machi 2008). Dennis Hopper – Republican Hopper considers a vote for Obama. ContactMusic.com. Retrieved 2010-05-29.
  3. Snead, Elizabeth (Jan/Feb 2001). "Dennis Hopper: Rennaissance Rebel". Cigar Aficionado. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-08. Iliwekwa mnamo 2009-11-12. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  4. "Social Security Death Index". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-12-09. Iliwekwa mnamo 2021-11-16.
  5. O'Hare, Cate (26 Oktoba,2005). "Hopper Evolves From Rebel to Republican". Zap2It.com. Tribune Media Services. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-28. Iliwekwa mnamo 2010-05-28. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help); Text ",00.html" ignored (help); Text ",00.html" ignored (help); Text "1" ignored (help); Text "1" ignored (help); Text "98259" ignored (help); Text "98259" ignored (help)