Nenda kwa yaliyomo

Denise Bucumi-Nkurunziza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Bucumi-Nkurunziza
Alizaliwa 1 Desemba 1969
Nchi Burundi
Kazi yake Waziri

Denise Bucumi-Nkurunziza (alizaliwa Gatsinda Mwumba, Mkoa wa Ngozi, 1 Desemba 1969) alikuwa Mke wa Rais wa Burundi kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2020, Pierre Nkurunziza. Ndiye Waziri pekee aliyewekwa rasmi ambaye amehudumu kama mke wa rais kitu ambacho hakijawahi tokea taifa lolote la Afrika.[1]

Denise Bucumi-Nkurunziza aliolewa na Pierre Nkurunziza mwaka 1994 muda mfupi kabla ya Nkurunziza kulazimishwa kwenda mafichoni katika hatua za mwanzo za Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Burundi. Baadaye aliingia katika Baraza la Kitaifa la waasi la Kutetea Demokrasia - Vikosi vya Kutetea Demokrasia (Conseil National Pour la Défense de la Démocratie - Forces pour la Défense de la Démocratie, CNDD-FDD) na akapanga safu zake za uongozi. Msururu wa makubaliano mwaka 2003 ulifungua njia kwa CNDD–FDD kuunganishwa tena katika siasa. Bucumi-Nkurunziza alirudiana tena na mumewe baada ya miaka kadhaa ya kutengana kwao.

Wote wawili Bucumi-Nkurunziza na mumewe walikuwa Wakristo wa Kanisa la Kiinjili la Waprotestanti.[2] Bucumi-Nkurunziza alikua Waziri aliyetawazwa na alihusika katika shughuli za hisani chini ya taasisi yake ya Buntu kama Mke wa Rais. Aliandika tawasifu, iliyochapishwa na L'Harmattan. Wenzi hao walijaaliwa kuwa na watoto sita pamoja.

Asubuhi ya tarehe 28 Mei mwaaka 2020, alisafirishwa kwa ndege hadi Nairobi, Kenya kutibiwa UVIKO-19 wakati wa janga la UVIKO-19 nchini Burundi. Alipelekwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan. Mumewe alifariki tarehe 8 Juni mwaka 2020 huko Karuzi. Ingawa sababu ya kifo ilisemekana kuwa mshtuko wa moyo, lakini ilishukiwa sana kwamba alikuwa amekufa kwa ugonjwa wa UVIKO-19.[3]

Uandishi

[hariri | hariri chanzo]

Denise Bacumi mnamo mwaka 2013 alitoa kitabu kinacho husu maisha yake kilicho andikwa na muandishi wa Ufaransa L'Harmattan

  • Nguvu ya Matumaini: Mke wa Rais wa Burundi. Hadithi Yangu (Paris: L'Harmattan, 2013).The Power of Hope: The First Lady of Burundi. My Story (Paris: L'Harmattan, 2013)
  1. "Mail & Guardian - Africa's Best Read". The Mail & Guardian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-18.
  2. "Burundi law to limit church numbers", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2014-07-10, iliwekwa mnamo 2022-03-18
  3. "Pierre Nkurunziza obituary". the Guardian (kwa Kiingereza). 2020-06-12. Iliwekwa mnamo 2022-03-18.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Denise Bucumi-Nkurunziza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.