Dawn Faith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dawn Faith mackay
Amezaliwa 16 January
Afrika kusini
Nchi Afrika kusini
Kazi yake muigizaji

'Maandishi ya kooze'Dawn Faith Mackay (née Mlotshwa, kuzaliwa KwaMashu, KwaZulu-Natal, Afrika Kusini, 16 Januari 1982) ni mwigizaji, mwimbaji muziki, mwanaharakati wa masuala ya kijamii, na mwendesha kipindi cha Deep & Meaningful.

Alianza kazi ya muziki mwaka 2008 akifanya kazi na msanii wa ndani kutoka Afrika Kusini na kuanzia hapo alitoa kazi yake ya kwanza kwa jina la "Audience of One" mwaka. Mnamo mwaka 2016, alianzisha kampuni ya kuzalisha maonyesho ya televisheni kwa jina la ‘’MYZIZI Productions’’, kwa heshima ya binti yake Zinhle (Zizi) Grace, ambaye alimzaa njiti wa miezi minne, na kufa akiwa na miei mitatu tu.[1] jijini Melbourne, Australia.

A New Dawn-21.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Mapenzi ya kuimba yalianza akiwa kanisa analosali bibi yake, kanisa hilo lipo katika mji wa KwaMashu, ambapo ndipo Mackay alikulia. Mapenzi ya muziki yalijengwa na mama yake, ambaye alipendelea kusikiliza nyimbo za Aretha Franklin, Donnie Hathaway na Kool & The Gang mapema alfajiri na pia usiku. Katika umri mdogo, Mackay alipata uzoefu wa nguvu ya muziki katika kuleta mabadiliko katika jamii, kwani ilikua katika nyimbo wakati wa kupinga ubaguzi wa rangi.

Harakati za Kijamii[hariri | hariri chanzo]

Akishawishika na malezi aliyopatiwa na matamanio yake ya kuleta mabadiliko katika jamii, Mackay amewekeza muda wake mwingi akihamasisha vijana kujikuza zaidi ya mazingira yao. Alikua mkurugenzi wa moja ya mashirika yanayoongozwa na vijana la ‘’Oaktree foundation’’ na kufanya kazi kwa ushirikiano na shirika la Nelson Mandela la ‘’46664’’ kutafuta namna ya kutumia muziki kuleta manufaa. Baada ya kuhamia nchini Australia mwaka 2009, alikuza harakati zake za kufuatilia haki, akifanya kazi kuwawezesha vijana wasio na uwezo pamoja na wahamiaji.

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Mackay amerekodi na kushirikiana na wasanii maarufu mbalimbali wa Afrika kusini (Loyiso Bala, Zakes Bantwini & Ntokozo Mbambo) na Australia (‘’Evermore band’’, ‘’Diafrix’’). Akiweza kuonyesha kipaji chake kama muimbaji na muandishi wa nyimbo, Mackay kwa sasa anatumia nyimbo zake kufikia na kuhamasisha watu kwote duniani. Mara nyingi amekua akialikwa kutumbuiza kwa kuimba pekee au pamoja na kundi katika matukio mbalimbali kama vile harusi, matamasha na wakati wa kutolewa tuzo mbalimbali. Amefanya maonyesho katika kumbimbali maarufu duniani kama vile Sydney Opera House, akiwa na wasanii mahiri kama Yvonne Chaka Chaka.

Wimbo wake wa kwanza, "Messed Up Heart", ulitengenezwa na Jason Heerah katika studio za Electric Empire na Dorian West wa ‘’The X Factor’’, ‘’Australia's Got Talent’’ – na kunsaidia Mackay kuwa msanii nambari 1 Melbourne na Nambari 7 Australia katika Chati za ‘’ReverbNation R&B/Soul’’. Ilifuatiwa na toleo lililotarajiwa na wengi la, "Audience of One", ambayo iliandikwa na kuandaliwa na Mackay mwenyewe. Katika hatua za kuondoka kwenye sauti ambazo kwa kawaida zimetawala muziki wa kikristo, toleo hilo lilikua na mkusanyiko wenye uainishaji lakini kufafanua uhalisia, ikichanganya miondoko ya jazz na muziki wa injili, ikiwa na mashairi yenye kufariji na kutia moyo. Ilihamasishwa na kifo cha binti yake, kuzaliwa kwa mtoto wake wa kiume na safari kati ya matukio haya mawili yaliyobadilisha Maisha yake.

Albamu[hariri | hariri chanzo]

Jina Maelezo ya Albamu
Audience of One
  • Kuachiwa: October 2015
  • Lebo: MYZIZI Music
  • Umbizo: Pakuo la digiti
Messed up Heart
  • Kuachiwa: October 2014
  • Lebo: MYZIZI Music
  • Umbizo: Pakuo la digiti
Black Harmony
  • Kuachiwa: June 2013
  • Lebo: MYZIZI Music
  • Umbizo: Pakuo la digiti

Kuongea[hariri | hariri chanzo]

Alishawahi kualikwa kushirikisha watu historia yake kama njia ya kutia hamasa vijana katika kumbi, makanisa na shule, ikiwemo shule ya uongozi mahususi kwa wasichana chini ya Oprah Winfrey.

Kazi za hivi karibuni[hariri | hariri chanzo]

Mackay alirudi Afrika Kusini mwaka 2016 kuandika na kuachia kitabu chake cha kwanxa kwa jina la, Dear God, ambacho kinaelezea historia ya marehemu binti yake na kwa jinsi gani Mackay alijiweka imara maada ya tukio hilo. Mradi wake mkubwa unaofuata ni kipindi cha maongezi kwa jina la ‘’Deep & Meaningful’’,[2] ambacho yeye mwenyewe ndiye aliyetunga na ndio muongozaji. Kipindi hicho kitaendeshwa na Mackat, na kitashirikisha wanawake tofauti wenye umaarufu kama wageni waalikwa, kitarushwa kwote Afrika kupitia chaneli ya BET Afrika namba 129.

Kwa sasa anaishi jijini Johannesburg pamoja na mume wake raia wa Australia bwana Nic Mackay wakiwa na mtoto wao wa kiume, Lwandle Mackay.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

[3][4] [5][6][7] [8][9]

  1. Eleftheriou, Krista. "The 2017 Annual Memorial Service". The Women's. 
  2. MALIBA, AMANDA. "Singer Dawn Faith takes on Deep & Meaningful task". Independent Online. South Africa: Independent News Online. Iliwekwa mnamo 22 August 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "The 2017 Annual Memorial Service". The Royal Women's Hospital. 
  4. "Zulu wedding for Nic and Dawn". Independent Online. South Africa. 
  5. "Zulu choir performs live". Australian Broadcasting Corporation. 26 August 2009.  Check date values in: |date= (help)
  6. "Seven Young Australians Changing the World -". ProBono Australiaprobonoaustralia.com.au. 
  7. "#48 with Dawn Faith - TBN Meets - Now available on demand". tbninafrica.org. 
  8. "Singer Dawn Faith takes on Deep & Meaningful task". article.wn.com. 
  9. "Singer Dawn Faith takes on Deep & Meaningful task". Independent Online. South Africa. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dawn Faith kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.