Das EFX
Das EFX | |
---|---|
Asili yake | Petersburg, Virginia, Marekani |
Aina ya muziki | Hip-Hop, hardcore hip hop |
Miaka ya kazi | 1988–hadi sasa |
Studio | East West Records/Atlantic Records |
Ame/Wameshirikiana na | EPMD, Hit Squad, DJ Premier |
Wanachama wa sasa | |
Dray Skoob |
Das EFX ni kundi la muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Kundi linaunganishwa na Ma-Emcee wawili ambao ni Skoob (anajulikana pia kama Books, amezaliwa na jina la William "Willie" Hines, mnamo 27 Novemba, 1970) na Dray (anajulikana pia kama Krazy Drayzy, amezaliwa na jina la Andre Weston, mnamo 9 Septemba, 1970). Wameanza kupata umaarufu wao mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa kufuatia kushirikiana kwao na kina EPMD na Hit Squad na kwa pamoja waliweza kueneza ladha ya mashairi ya ukweli, ambapo wakawa miongoni mwa wana hip hop waliokuwa na athira kubwa katika muziki wa hip hop mwanzoni mwa miaka ya 1990.[1] Staili yao inajumlisha mistari ambayo si mibaya sana ambayo wanaimba kwa kasi sana (ikiwa ni pamo mwisho wake kutia maneno kama "-iggedy") na marejeo kadha wa kadha za tamaduni maarufu.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mwanachama Skoob anatoka mjini Brooklyn, New York City wakati Krazy Drayzy anatoka mjini Teaneck, New Jersey lakini wawili hao walikutana katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Virginia kunako mwaka wa 1988 na wakaanza kuimba pamoja. Wamejiita "Das" inasimama kama "Drayz na Skoob" na "EFX" ina maana ya "effects". Das EFX wamepata mwamko wa kina EPMD katika onesho moja la kusaja watu wenye vipaji, licha ya kupoteza shindano, wamefanya vyema kiasi cha kuwashawishi kina EPMD kuingia nao mkataba wa kurekodi. Wawili walipata umaarufu na mafanikio yao makubwa baada ya kutoa albamu yao ya kwanza , Dead Serious, ambayo iliangaza staili yao ya kurap ambayo si ya kawaida ambayo waliita jina la "sewage".
Dead Serious ikabahatika kwenda katika ngazi ya platinum na kibao chake kikali cha, "They Want EFX," (ambayo ilichukua sampuli kadhaa za kibao cha James Brown "Blind Man Can See It" na kingine cha Malcolm McLaren "Buffalo Gals") kilifika katika chati za kumi bora ya Billboard na R&B huko nchini Marekani, arobaini bora ya Billboard Hot 100 na #1 kwenye chati za Hot Rap Tracks. Zikifuatiwa na single kama vile "Mic Checka" na "Straight Out the Sewer" hazijashika chati kabisa kwenye Hot 100, lakini zilifika nafasi ya #1 na #3 kwenye chati za Hot Rap Tracks.
Wawili hawa walipata kuonekana kwenye single bab-kubwa ya Ice Cube "Check Yo Self". Wimbo huo ulifika nafasi ya #20 kwenye chati za Hot 100 na #1 kwenye Rap Tracks. Wimbo ulishika nafasi ya #36 kwenye chati za UK Singles Chart mnamo mwezi wa Agosti 1993. Single hii pia iliuza zaidi ya nakala milioni moja nchini Marekani.[2] Their refrain of "Chiggedy-check yo self before you wriggedy-wreck yo self" became a catchphrase in 1993. The song has since appeared in the videogame Grand Theft Auto: San Andreas, playing on the radio station Radio Los Santos.
Kipindi ambacho kundi li linaanza mnamo 1992 hadi 1993, mitindo yao kadha wa kadha ilipatwa kuigwa na baadhi ya makundi mengine ya muziki wa hip hop kama vile Lords of the Underground, The Fu-Schnickens, Kris Kross, Common na hata, hasa kidogo Public Enemy. Mtindo wao wa iggedy nao ulipatwa kurudiwa tena mnamo mwaka wa 1996 na BLACKstreet kwenye wimbo wao wa "No Diggity" wakiweka "diggity" wakimaanisha "doubt" au "shaka". Hii pia ulikuwa moja kati ya misemo maarufu sana kwa kipindi hicho.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Maelezo ya Albamu |
---|
Dead Serious
|
Straight Up Sewaside
|
Hold It Down
|
Generation EFX |
How We Do
|
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Das EFX katika MySpace
- Interview with Das EFX from 2003 Archived 1 Januari 2006 at the Wayback Machine.
- Interview with Das EFX from 2007 Archived 2 Februari 2010 at the Wayback Machine.
- Krazy Drayzy 2009 Interview (ArtofRhyme.com) Archived 7 Julai 2011 at the Wayback Machine.
- Das EFX international fun club Archived 14 Agosti 2011 at the Wayback Machine.