Nenda kwa yaliyomo

Daniel W. Dobberpuhl

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Daniel "Dan" William Dobberpuhl - (25 Machi 1945 - 26 Oktoba 2019[1]) alikuwa Mhandisi wa Umeme nchini Marekani ambaye aliongoza timu kadhaa za wabunifu wa maikroprosesa

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Dobberpuhl alizaliwa tarehe 25 Machi 1945 huko Streator, Illinois. Mnamo mwaka 1967,Alihitimu shahada ya Sayansi katika uhandisi wa umeme kutoka Chuo Kikuu cha Illinois huko Urbana-Champaign. Alifanya kazi kama mhandisi wa Idara ya Ulinzi hadi mnamo mwaka 1973, Alipofanya kazi katika Kampuni ya General Electrical (GE) huko Syracuse, New York.

Mnamo 1976 Dobberpuhl alijiunga na kampuni ya Digital Equipment Corpartion (DEC) huko Hudson, Massachusetts kama mhandisi wa semicondukta na aliongoza timu ya ubunifu wa maikroprosesa kama vile DEC T-11 na MicroVAX. Alipanda nafasi za juu zaidi za kiufundi katika Kampuni ya DEC na kuwa mmoja wa wahandisi watano wakuu wa ushauri wa kampuni hiyo. Hata hivyo, aliongoza timu ya ubunifu kwa vizazi vitatu vya kwanza vya prosesa (CPU) ya DEC Alpha na mnamo mwaka1985 alichapisha kitabu kilichoitwa " The Design and Analysis of VLSI Circuits ", kilichoelezewa kama "maandishi yatakayo ongoza sekta ya umeme."[2]

  1. "Daniel Dobberpuhl Obituary (1945 - 2019) Monterey Herald". Legacy.com. Iliwekwa mnamo 2022-08-01.
  2. "Current IEEE Corporate Award Recipients". IEEE Awards (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-08-01.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Daniel W. Dobberpuhl kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.