Bongo kuu (kompyuta)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
CPU ya Intel

Bongo kuu (pia Kitengo kikuu cha uchakataji[1]; pia: CPU, kifupi cha Kiingereza "central processing unit") ni sehemu muhimu ya tarakilishi.

Ni kweli bongo la mashine hiyo kwa sababu kila sehemu ya tarakilishi inahitaji CPU kwa njia fulani ikitekeleza shughuli zake.

Ina sehemu tatu ambazo ni muhimu kwa utendakazi wake. Nazo kwa Kiingereza zinaitwa:

  1. Arithmetic Logic Unit (ALU)
  2. Control Unit
  3. Main Memory

Arithmetic Logic Unit (ALU)[hariri | hariri chanzo]

Hii ni sehemu muhimu ya bongo kuu inayoandaa taarifa zote za kihisabati. Taarifa hizi zaweza kuwa hesabu za kujumlisha au kutoa.

Control unit[hariri | hariri chanzo]

Sehemu hii ya Bongo Kuu inaratibu vifaa vyote vinavyoingiza na kutoa taarifa mbalimbali katika kompyuta. Vifaa hivi vyaweza kuhusisha scrini, bao bonye, puku au kipanya, machine ya kutoa nakala, mashine ya kuingiza nakala ya taarifa kwenye kompyutya na nyinginezo nyingi.

Kumbukumbu kuu[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida bongo kuu huhitaji kiasi fulani cha kumbukumbu ambayo hurahisisha uhifadhi wa taarifa mbalimbali mara zinaposubiri nafasi ya kuweza kuwekwa katika hali ya mchakato kuziwezesha taarifa hizo kutoa matokeo yaliyokusudiwa. Sehemu hii ni ya muhimu zaidi kwani hurahisisha kazi ya bongo kuu na kuiwezesha kutoa matokeo yaliyokusudiwa kwa muda mfupi kwa kupunguza umbali na muda wa kuzihusisha taarifa mbalimbali wakati wa mchakato

Utengenezwaji[hariri | hariri chanzo]

Bongo kuu ni kifaa muhimu na chenye gharama kubwa hivyo utenenezwaji wake ni wa gharama kubwa. Sio kila mtu anauwezo wa kuzitengeneza hivyo basi ni makampuni machache yenye uwezo wa kutengeneza. Makampuni haya yanajumisha intel, AMD, POWERPC na nyinginezo.

Upatikanaji[hariri | hariri chanzo]

Upatikanaji wa bongo kuu unategemea kasi, ukubwa wa mchakato wa data, pamoja na bei na unaweza kuzinunua popote pale kwenye maduka ya spea za kompyuta. Pia unahitajika kujua muingiliano wa bongo kuu ya kompyuta unayoitumia na spea utakayoinunua kabla hauja inunua kwani haitaweza kufanya kazi ipasavyo ikiwa kutakuwa na utofauti baina ya bodi mama na bongo kuu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. hivyo orodha ya Kilinux (2009) na pia KSK (2011)