Nenda kwa yaliyomo

Buku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cricetomys)
Buku
Buku-misitu (Cricetomys emini)
Buku-misitu (Cricetomys emini)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Nesomyidae (Wanyama walio na mnasaba na buku)
Forsyth Major, 1897
Nusufamilia: Cricetomyinae (Wanyama wanaofanana na buku)
Roberts, 1951
Jenasi: Beamys Thomas, 1909

Cricetomys Waterhouse, 1840
Saccostomus Peters, 1846

Mabuku ni wanyama wa nusufamilia Cricetomyinae katika familia Nesomyidae ambao wanafanana na panya, lakini panya ni wanafamilia wa Muridae. Mabuku ni wakubwa kiasi, pengine kushinda panya: wale wa Cricetomys wana mwili wa sm 25-45, mkia wa sm 36-46 na uzito wa kg 1-1.5; wale wa Beamys wana mwili wa sm 13-19, mkia wa sm 10-16 na uzito wa g 55-150; na wale wa Saccostomus wana mwili wa sm 9.5-19, mkia wa sm 3-8 na uzito wa g 40-120. Wana pochi kwa ndani ya mashavu yao ambazo wazitumia kwa kuweka chakula. Hula mbegu, matunda, makokwa, mizizi na wadudu na hupenda machikichi sana. Rangi yao ni kijivu au kahawia juu na nyeupe chini.