Cool Runnings

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cool Runnings

Bango kwa ajili ya toleo la sinema
Imeongozwa na Jon Turteltaub
Imetayarishwa na
Imetungwa na
Nyota
Muziki na Hans Zimmer
Sinematografi Phedon Papamichael
Imehaririwa na Bruce Green
Imetolewa tar. Oktoba 1, 1993 (1993-10-01)
Ina muda wa dk. 98 minutes
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu $14 million
Mapato yote ya filamu Dola milioni 154.9 za Marekani

Cool Runnings ni jina la filamu ya michezo-vichekesho iliyotolewa mwaka 1993 huko nchini Marekani. Filamu imeongozwa na Jon Turteltaub, na kuchezwa na Leon, Doug E. Doug, Rawle D. Lewis, Malik Yoba na John Candy. Filamu ilitolewa nchini Marekani mnamo tarehe 1 Oktoba, 1993. Hii ilikuwa filamu ya tatu ya mwisho ya kazi kuigiza kwa Candy na filamu ya mwisho kutolewa akiwa hai. Hii inatokana na hadithi ya kweli ya timu ya taifa ya bobsledi ya Jamaika ilipoingia kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Olimpiki ya Majira-Baridi ya 1988 huko mjini Calgary, Alberta, Canada.[1][2] Filamu imepokea tahakiki chanya, na kibwagizo cha filamu nahco kimekuwa maarufu sana kwa Jimmy Cliff kurudia wimbo wa "I Can See Clearly Now" na kufikia nafasi ya 40 ikiwa kama single huko nchini Canada, Ufaransa, na Uingereza.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Derice Bannock, mkimbiaji maarufu wa mbio za mita 100, ameshindwa kufudhu katika Majaribio ya Olympic kwa ajili ya Mashindano ya Olympic ya Kiangazi ya 1988 pale mkimbiaji mwenza Junior Bevil alipoteleza na kuanguka, huku akiwaangusha wenziwake kina Derice na mkimbiaji mwenginer, Yul Brenner, wote wameenda chini.

Ili waweze kushindana katika mashindano ya Olympics, yeye na rafiki yake wa karibu, Sanka Coffie, bingwa wa kukimbiza kigari cha kubeba vingoe, wameenda kumwomba Irv Blitzer, rafiki wa zamani wa baba yake Derice Mzee Ben ambaye awali alijaribu kuwakusanya wakimbia mbio kujiunga na uanzishwaji wa timu ya bobsledi miaka kadhaa iliyopita. Irving ni Mmarekani aliyeshinda Medali ya Dhahabu katika bobsledi mara mbili katika Mashindano ya Olympic ya Majira Baridi 1968 ambaye alimaliza maonesho mawili na tena katika kipindi cha Olympic ya 1972 lakini alitolewa ushindi hapo baadaye hasa kwa kudaiwa amedanganya na kustaafu kwa fedheha huko Jamaica, ambako anaishi maisha ya ovyo kabisa akiwa kama mtu wa kubeti (mkusanya pesa za mashindano na bahati nasibu katika michezo). Ung'ang'anizi wa Derice hatimaye ukamshawishi Irving kuwa kocha wao na kurudia maisha aliyoyaacha nyuma. Hatimaye wakamwingiza Junior na Yul, japokuwa Yul bado yu na hasira dhidi ya kosa la Junior katika Majaribio ya Olympic.

Wanne wale walitumia njia mbalimbali kujitafutia pesa kwa ajili ya safari ya kwenda katika mashindano ya Olympics lakini hakuna mfadhili aliyechukulia wazo la uzito wowote ule licha ya kuwa na mabiashara kadhaa. Kutokana na hilo, wakajiongeza kila mtu afanye kitu cha kutupatia pesa, wengine mchezo wa miereka ya mkono, kibanda cha kupigia madenda, yote wamefeli. Junior anakuja na mapesa aliyouza gari lake, pesa ambazo zimeweza kusaidia timu kiasi walichohitaji. Baadaye katika chumba cha hoteli Junior anamkaripia Sanka kwa kuumiza hisia za Yul kuhusu malengo makuu yake. Junior anaieleza timu kuhusu baba yake mzazi alivyoanza kuhangaika na maisha ya chini kabisa leo hii anaishi katika jumba la kifalme. Anamtia moyo Yul hasikate-tamaa katika kutimiza malengo yake na tangu hapo wawili hao wakaanza kuheshimiana.

Huko Calgary, Irving anafanikisha kupata kisleji cha kale kwa ajili ya mazoezi, kwa vile Wajamaika hawakuwa katika orodha ya halisi ya bobsledi. Wajamaika walidharulika kila waendapo na watu kutoka nchi nyingine, hasa kikosi cha Wajerumani Mashariki ambacho kiongozi wao kiburi, Josef, anawaambia waende kwao, hili lilipelekea mbilinge na mapigano baa baadaye. Wakiwa chumba cha hoteli, Derice wanamkemea Sanka, Yul na Junior anawakumbusha kipi kipo hatarini kwa kikosi. Kikosi kimeazimia kuchukulia shindano kwa uzito, wakaendelea kujifunza ili kuboresha mbinu zao. Wamefudhu mashindano, lakini baadaye wakafanyiwa hila na kutolewa kwa kufuatia sababu za kiufundi ambazo kamati ya Olympic iliona inafaa hasa kwa kufuatia kashfa ya Irving ya kudanganya. Irving aliyevurugwa kavamilia kikao cha kamati na kumshambulia kocha wake wa zamani wa 1972 Olympic Kurt Hemphill, sasa ni jaji mkuu katika Mashindano ya 1988. Amewajibika kwa fedheha aliyoipatia nchi yake na kuitaka kamati imuadhibu yeye kwa makosa yake, lakini si timu ya Jamaika. Irv anawakumbusha ya kwamba Wajamaika wanastahili kuwakilisha nchi yao katika Mashandano ya Baridi wakiwa kama washidani. Usiku ule hotelini, timu inapokea simu inayotaarifu ya kwamba kamati imerejesha uamuzi wao juu ya kushindana kwa kikosi cha Wajamaika, hivuo basi wamekubaliwa kushiriki.

Siku ya kwanza ya Wajamaika ilikuwa fedheha tupu na kuishia kuwa mwisho kumaliza. Sanka anatambua shida ni kwamba Derice anajaribu kunakili kikosi cha Waswiss na kumperemba ya kwamba njia pekee na nzuri ni kubobsledi Kijamaika tu na vingine. Pindi tu kikosi kilipounda mtindo wao wenyewe na wa kinyumbani, siku iliyofuata wameboreka; kikosi cha Wajamaika wanamaliza kwa spidi kubwa huku wakiwa nafasi ya nane. Derice anamwuliza Irving kuhusu kwanini kadanganya licha ya kuwa medali ya dhahabu tayari ni fahari; Irving anamweleza Derice, "Medali ya dhahabu ni kitu kizuri, lakini kama hukamiliki bila kuwa nayo, kamwe hutotosheka kuwa nayo," na kumshawishi ajione ni mshindi hata kama atashindwa kuchukua dhahabu.

Siku kwanza tu ilionekana kama vili kikosi hiki kitavunja rekodi ya dunia katika mashindano ya bobsledi kwa mara ya kwanza kwa kasi, hadi hapo ilipotokea tatizo la kusikitisha: hasa kwa kufuatia kile kisleji kuwa cha kale sana, hakiwezi kuhimili mwendokasi na hatimaye kengee/msume-bapa ukalegea, ukasababisha kibinuke kiupandeupande huku kikiwa kinatoka katika mzunguko, huku ikiabakisha mita kadhaa tu kwa kikosi kumaliza. Wakaazimia kumaliza mashindano kwa hali yoyote ile, kikosi kikainua sleji juu begani na kutembea mule katika zile za sleji huku makofi kwa wifi wakifuatia kutoka kwa watazamaji na wakaguzi, akiwemo Josef, Hempill, na babake yake Juniorr. Kikosi mwishoni, walijisikia furaha ya kutosha kurudia tena katika mashindano hayo miaka minne ijayo. Duru zinasema walirudi nchini Jamaika wakiwa kama mashujaa - pamoja na kurudi kwao tena katika Olympic ya 1992, walichukuliwa sawa na wengine bila kubughudhiwa.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Kibwagizo cha filamu kilitolewa na Sony mnamo 1993 kwenye CD (Columbia Chaos OK 57553).

Katika baadhi ya nchi za Ulaya kibwagizo kilitolewa na Sony zikiwa na nyimbo za ziada 12 (bonasi) moja wapo ikiwa Rise Above It iliyoimbwa na Lock Stock na Barrel (Columbia 474840 2). Nyimbo kutoka katika kibwagizo zimeonekana katika filamu ikiwa ni pamoja na "Rasta in the Snow", ambao ulitokana na kikosi halisi cha bobsledi cha Jamaika.

No. JinaMuziki Urefu
1. "Wild Wild Life"  Wailing Souls 3:36
2. "I Can See Clearly Now"  Jimmy Cliff 3:16
3. "Stir It Up"  Diana King 3:49
4. "Cool Me Down"  Tiger 3:50
5. "Picky Picky Head"  Wailing Souls 4:10
6. "Jamaican Bobsledding Chant"  Worl-A-Girl 4:16
7. "Sweet Jamaica"  Tony Rebel 3:51
8. "Dolly My Baby"  Super Cat 3:32
9. "The Love You Want"  Wailing Souls 3:59
10. "Countrylypso"  Hans Zimmer 2:48
11. "The Walk Home"  Hans Zimmer 4:37
12. "Rise Above It" (bonus track included only on European release reference number 474840 2)Lock Stock and Barrel 3:32

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: