Wingu vundevunde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cirrus cloud)
A photograph showing many types of cirrus clouds all jumbled together floating above a plain
Anga iliyojaa aina mbaimbali za mawingu vundevunde

Wingu vundevunde (kwa Kilatini/Kiingereza: cirrus, "shungi la nywele") ni wingu la fuwele za barafu linalopatikana kwa kimo kikubwa. Mawingu vundevunde huonekana kama nyuzi nyeupe au kanda nyembamba angani[1].

Mawingu hayo hutokea kwenye kimo cha mita 16,500 hadi 45,000.

Kutoka kwenye uso wa Dunia, mawingu vundevunde huonekana kuwa na rangi nyeupe au kijivu. Yanaundwa wakati mvuke wa maji hupitia kimo cha mita 5,500 ambako baridi huongezeka, hivyo mvuke unaganda na kuunda fuwele za barafu.

Kwa kawaida kimo cha mawingu hayo ni mita 8,000–12,000 juu ya usawa wa bahari.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Funk. Cloud Classifications and Characteristics. The Science Corner. National Oceanic and Atmospheric Administration. Iliwekwa mnamo 30 January 2011.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wingu vundevunde kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.