Nenda kwa yaliyomo

Mkesha-maji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cinclidae)
Mkesha-maji
Mkesha-maji wa Ulaya
Mkesha-maji wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege waimbaji)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Cinclidae (Ndege walio na mnasaba na mikesha-maji)
Jenasi: Cinclus
Borkhausesn, 1797
Ngazi za chini

Spishi 5:

Mikesha-maji ni ndege wadogo kiasi wa familia Cinclidae wafananao na mikesha wadogo. Katika Afrika wanatokea Milima ya Atlas huko Maroko. Wana mkia mfupi na mabawa mafupi yenye nguvu. Ndege hawa hutafuta chakula majini na waweza kuingia maji wakizama kabisa. Kwa hivyo miguu yao ni mirefu yenye makucha makali ili kushikilia mawe ndani ya maji matiririkayo. Pia hutumia mabawa yao mafupi kama aina za mapezi. Hula lava na viluwiluwi vya wadudu wa maji hasa lakini samaki wadogo, mayai ya samaki, makoa na gegereka pia. Tago lao kubwa hujengwa kwa vigoga karibu na maji katika shimo lo lote au chini ya daraja. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi ya Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]