Chusa

Chusa ni kifaa kirefu chenye umbo la mkuki kinachotumiwa kwa shughuli za uvuvi na uwindaji wa wanyama wa majini.
Mara nyingi chusa imefungwa kwa kamba inayoruhusu mvuwi kuirudisha pamoja na windo.
Ncha za chusa za samaki kwa kawaida huwa na vipembe vikali vidogo vya kuelekea nyuma. Hivi vinaingia ndani ya mwili wa windo na kuizuia isitoroke.
Chusa zilipatikana tangu zama za mawe. Zamani na kimapokeo zilitengenezwa mara nyingi kwa kutumia ubao au mifupa iliyokatwakatwa kwa kupata vipembe vya kuelekea nyuma. Siku hizi ncha ni za metali.
Chusa zilitumiwa pia kama silaha. Katika michezo ya Roma ya Kale kulikiwa na magladiator walioitwa "wavuwi" waliotumia nyavu na chusa kama silaha zao.
Picha[hariri | hariri chanzo]
- Chusa katika historia
Chusa mbalimbali za mfupa, zama za mawe
Chusa ya chuma yenye ncha 3, Roma ya Kale
Unaaq, chusa ya Eskimo
Chusa ya kisasa kwa uvindaji nyangumi