Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (au kiing.: Teofilo Kisanji University) ni chuo kikuu chipukizi kinachokua haraka katika mji wa Mbeya (Tanzania) kinachopatikana tangu mwaka 2005. Kinatoa kozi kwenye vitivo au idara nne za

  1. Ualimu (Faculty of Education)
  2. Teolojia (Faculty of Theology)
  3. Fani za sanaa na Sosholojia (Faculty of Arts and Social Science)
  4. Sayansi na Teknolojia (Faculty of Science and Technology)

Chuo chasimamiwa na Kanisa la Moravian Tanzania.

Chuo kipo Mbeya mjini katika eneo la "Block T" karibu na uwanja wa ndege wa mjini eneo la Soweto/Mwanjelwa.

Jina

Jina la chuo kikuu limeteuliwa kwa heshima ya Teofilo Kisanji (1915-1982) aliyekuwa askofu wa kwanza Mwafrika wa Kanisa la Moravian Tanzania.

Historia

Chuo kikuu kilitanguliwa na Motheco kilichowahi kufundisha wachungaji pekee tangu 1969.

Chuo Kikuu kilianzishwa rasmi katika Agosti 2005 kwa idara ya theolojia pekee. Tangu Agosti 2006 idara ya ualimu ilianza kazi yake katika kozi za ualimu wa lugha.

Utawala

VC Dr Ntuli Kassimoto. DVCAA Dr Mosses. DVPF Mr Mabuga(ma)

Wahadhiri

Chuo kinawahadhiri wa ndani na nje mfano wake ni profesa Mwamwenda (Afrika Kusini), profesa Mbonile (UDSM), wengine ambao ni wakudumu ni Dr Ntuli, Dr Kouh, Dr Keryy, Dr moses, Dr Nzowa, Dr Zamuel, Mr Andersen (ma), Mr Alawi (ma), Mr Madulu (ma), Mr Ntonge (ma), Mr Kandoro (ma), Mr Mwasandube(ma), Mr Mwakilembe (ma),mr Haukila(ma), Mr Bakari(ma), Mr Nchimbi (ma),Mr Mahala (ma),Mr Mwakipesile (ma), Mr Mabuga (ma),Mr Mwambo (ma),Rev Kasyele(ma),Mrs Zamuel (ma),Mr Mwenisongole (ma), Mrs Ktegile(ma), Miss Stella(ma),Miss Lawi (ma), Miss Ndihesya (ma),Rev Meza, Ms Kategile,Rev Mbao.

Marejeo ya nje

Tovuti rasmi