Moravian Theological College

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Motheco)
Jump to navigation Jump to search

Moravian Theological College (Motheco) ilikuwa Chuo cha Theolojia cha Kanisa la Moravian Tanzania katika mji wa Mbeya (Tanzania).

Kilianzishwa Chunya mwaka 1969 na kuhamia Mbeya mwaka 1978.

Kilifundisha wachungaji wa Kanisa la Moravian Tanzania pia wa Kilutheri hadi kiwango cha cheti na diploma.

Mwaka 1990 kozi ya BD (Bachelor of Divinity) ilianzishwa.

Tangu 2005 Motheco ilikwisha kwa kuingia katika Chuo Kikuu Teofilo Kisanji.