Teofilo Kisanji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Teofilo Hiobo Kisanji (26 Desemba 1915 - 15 Aprili 1982) alikuwa mwalimu, mchungaji na baadaye askofu Mwafrika wa kwanza wa Kanisa la Moravian Tanzania.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kisanji alizaliwa katika kijiji cha Chadodwa kwenye wilaya ya Sikonge katika familia ya Wanyamwezi Wakristo. Baba alikuwa mwinjilisti wa kanisa la Moravian. Akasoma ualimu akafundisha shuleni tangu 1933 na baadaye kama mwalimu wa chuo cha ualimu.

Mwaka 1949 akafuata wito wa kuwa mchungaji wa kanisa akibarikiwa 1950. Alisoma theolojia huko Uingereza na Uholanzi akarudi Tanzania kuwa mchungaji Tabora mjini.

Mwaka 1962 alichaguliwa kuwa mchungaji kiongozi kwa cheo cha "superintendent" akiwa Mwafrika wa kwanza katika kanisa lake. 1965 akateuliwa kuwa askofu Mwafrika wa kwanza katika kanisa la Moravian Tanzania akasimamia jimbo la Tanzania Magharibi (Tabora). Alikuwa askofu wa Moravian Mwafrika wa pekee nchini Tanzania hadi 1979.

Kisanji alikuwa kati ya viongozi wa makanisa waliojenga umoja wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). Mwaka wa 1968 alishiriki katika azimio la kuanzisha chuo cha Motheco mjini Chunya. Aliandika vitabu viwili juu ya historia ya kanisa la Moravian.

Kisanji alioa akazaa watoto 15 na mke wake Perpetua.

Aliaga dunia 1982 katika hospitali ya KCMC (Kilimanjaro Christian Medical Centre) mjini Moshi akazikwa Tabora.

Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji mjini Mbeya na Bishop Kisanji Women’s Centre mjini Morogoro vimepewa majina kwa heshima yake.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Teofilo Kisanji kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.