Catherine Ruge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Catherine Ruge (alizaliwa Juni 25, 1982)[1] ni mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya chama cha CHADEMA akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Macha aliyefariki dunia 21 Machi 2017.[2].

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alisoma Shule ya Sekondari Msalato mkoani Dodoma kuanzia mwaka 2001 hadi 2003. Baadaye alisoma Jangwani kuanzia Juni 2001 hadi Mei 2003 na kuhitimu elimu ya juu ya sekondari. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 2004 hadi 2007 akisomea Shahada ya Biashara na Uhasibu. Mwaka 2011 – 2015 alisoma Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara katika chuo cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute). Kwa sasa anachukua masomo ya udaktari (PHD) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye masuala ya jinsia katika fani ya uhasibu.[3]

Harakati za kisiasa[hariri | hariri chanzo]

Alijiunga na Chadema mwaka 2010 na ilipofika mwaka 2013 mwishoni alianza rasmi harakati za siasa.Alianza kwa kugombea nafasi ya katibu wa rasilimali fedha Kanda ya Serengeti na kushinda.[4]

Tarehe 04 Mei, 2017 aliteuliwa na NEC kuwa Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya chama cha CHADEMA kwa kuchukua nafasi ya Dr Elly Marco Macha.[5] [6][7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]