Nenda kwa yaliyomo

Catherine Apalat

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Catherine Apalat
Apalat mnamo 2018
Apalat mnamo 2018
Jina la kuzaliwa Catherine Apalat ,
Alizaliwa 28 Agosti 1981 ,Uganda
Kazi yake mwandishi wa habari

Catherine Apalat (alizaliwa Tororo, Uganda, 28 Agosti 1981) ni mwanahabari, mtayarishaji wa filamu na mpiga picha wa Uganda, “Media Women's Association” (UMWA).[1] Mnamo Aprili 2013, Apalat alikuwa meneja wa programu ya Mama FM iliyo chini ya UMWA.[2]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Apalat alizaliwa na David Livingstone Ongadi, mwalimu wa shule ya msingi, na Grace Onyadi, mtaalamu wa masuala ya mawasiliano. Apalat aliudhuria shule ya msingi iitwayo Rock View hadi mnamo mwaka 1994 kabla ya kujiunga na Tororo Girls, na baadaye shule ya “Our Lady of Gayaza” kwa ajili ya elimu yake ya sekondari mnamo mwaka 1995-2000. Apalat alisoma Makerere University na kutunukiwa shahada ya uzamili katika masuala ya mawasiliano mnamo mwaka 2005.

Apalat alifanya kazi na Makerere University kwenye idara ya mawasiliano na uandaaji wa filamu mnamo mwaka 2002. Apalat alitengeneza filamu fupi kumi za dakika kumi za kuchekesha na kiubunifu kama vile "Salongo’s Gift" na "Portrait of an artist". Apalat alijiunga na Radio kubwa na kufanya kazi kwenye idara ya utangazaji wa habari,uandaaji,uhariri na iliyobobea na utangazaji wa maswala ya jinai mwaka 2003. Apalat alijiunga na “the Great Lakes Film Production” mwaka 2005-2006 ambapo alifanya kazi kama mwandishi wa stori na mwendelezaji filamu.

Toka mwaka 2007 mpaka sasa, Apalat anafanya kazi kama mtayarishaji wa filamu na mpiga picha kwenye kituo cha “Uganda Media Women’s Association Newspaper pull out (The Other Voice) na “Grass Root Women Empowerment Network (GWEN) Magazine”. Apalat alifanya kazi kama mshiriki wa Fredskorpset (FK) na (Norway Peace Corp) pamoja na Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano (CJMC FM) mnamo 2011, uko Nepal. Wizara ya Mawasiliano ya Nepali, Nepal ilitambua mchango wa Apalat katika kuonyesha mila na tamaduni tofauti za Kiafrika kupitia filamu katika tamasha la kwanza la filamu la Nepal Afrika mnamo Mei 2011.[3][4][5]

Mpaka Aprili 2013, Apalat alikua ni mkurugenzi wa Programu kwenye Kituo cha Redio ya Jamii “Mama Fm”, huko Uganda.[2] Apalat ilifanya kazi na wafanyakazi wa redio hiyo kuhakikisha kuwa dhamira ya redio inazingatiwa pia inazalisha programu zinazozingatia jinsia, ujumbe wa matangazo na maigizo.

Apalat ameshiriki katika miradi kadhaa ya utafiti ikiwa ni pamoja na "“[[Grass roots Women in Technology]] mnamo 2013, uchambuzi wa Hadhira kwa wasikilizaji wa Mama FM mnamo 2014 na Mradi wa Ufuatiliaji wa Vyombo vya Habari Duniani (GMMP) mnamo 2015 na Chama cha Wanawake Vyombo vya Habari nchini Uganda.[1]

  1. 1.0 1.1 UMWA, UMWA (2016). A Gender Analysis Report on media and Elections. Kampala: UMWA. uk. 18.
  2. 2.0 2.1 "UGANDA MEDIA WOMEN'S ASSOCIATION & MAMA FM" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-06-26.
  3. Nepal Film Festival, Nepal Film Festival. "Media Coverage - Nepal Africa Film Festival". www.nepalafricafilmfestival.com.np. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-28. Iliwekwa mnamo 2020-06-25. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)
  4. "Faces of FK media women". Uganda Media Women's Assocaition (kwa Kiingereza). 2013-01-18. Iliwekwa mnamo 2020-06-25.
  5. "Gallery - Nepal Africa Film Festival". www.nepalafricafilmfestival.com.np. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-25. Iliwekwa mnamo 2020-06-25. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Catherine Apalat kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.