Castor na Pollux
Castor na Pollux walikuwa mapacha katika Mitholojia ya Kigiriki na mitholojia ya Kiroma. Pamoja wanaitwa Dioscuri . Walikuwa wana wa malkia Leda wa Sparta. Dada zao walikuwa mabinti mapacha Helena wa Troia na Klitemnestra . Castor na Pollux walibadilishwa kuwa kundinyota linalojulikana kwa jina Mapacha (ing. Gemini).
Ingawa walikuwa mapacha walizaliwa na mababa wawili tofauti: Baba wa Castor alikuwa binadamu Tindareus, mfalme wa Sparta na hivyo Castor alikuwa binadamu pia akijulikana atakufa, wakati baba wa Pollux alikuwa mungu Zeus kwa hiyo alikuwa na tabia ya kimungu asiyeweza kufa. Katika masimulizi ya Wagiriki mama Leda alilala na mumewe na siku ileile alitongozwa na Zeus kuzini naye ilhali Zeus alifika kwa umbo la batamaji.
Moja ya hadithi maarufu zaidi kuhusu Castor na Pollux ni jinsi walivyopelekwa angani kuwa kundinyota. Wakati wa vita fulani Castor mwenye tabia ya kibinadamu aliuawa. Pollux alihuzunika kupita kiasi akamwomba Zeus amfanye Castor asife ambayo ilimaanisha Pollux atalazimika kukupungukiwa tabia yake ya kimungu. Hatimaye, Zeus alikubali ombi hilo, kwa kuwapeleka wote wawili angani kama nyota. Walipangwa kukaa nusu mwaka kenye mlima Olimpos pamoja na miungu wengine lakini nusu mwaka wangekaa katika himaya ya mauti.
Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- "The Divine Twins in early Greek poetry". Robbins, Emmet. Thalia Delighting in Song: Essays on Ancient Greek Poetry. University of Toronto Press. 2013. pp. 238-253. ISBN 978-1-4426-1343-0
- Lippolis, Enzo. "RITUALI DI GUERRA: I DIOSCURI A SPARTA E A TARANTO." Archeologia Classica 60 (2009): 117-59. www.jstor.org/stable/44367982.
- De Grummond, Nancy Thomson. "Etruscan Twins and Mirror Images: The Dioskouroi at the Door." Yale University Art Gallery Bulletin, 1991, 10-31. www.jstor.org/stable/40514336.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Wikisource has the text of the 1911 Encyclopædia Britannica article Castor and Pollux. |
- Images of the Castor and Pollux in the Warburg Institute Iconographic Database Ilihifadhiwa 3 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.