Carolyn McCarthy
Mandhari
Carolyn McCarthy (amezaliwa Januari 5, 1944) ni muuguzi na mwanasiasa wa Marekani ambaye aliwahi kuwa mwakilishi wa bunge la New York kuanzia 1997 hadi 2015. Yeye ni mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia.
Mnamo 8 Januari 2014, alitangaza kwamba hatagombea tena katika uchaguzi wa Novemba, akastaafu mnamo Januari 2015 na nafasi yake ikachukuliwa na Mwanademokrasia mwenzake Kathleen Rice.