Caroline Ndosi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Caroline Ndosi
Caroline Ndosi.jpg
Jina la kuzaliwa Caroline
Nchi Tanzania


Caroline Ndosi (au: Carol Ndosi; amezaliwa tar.) ni mwanamke mjasiriamali Mtanzania mwenye uzoefu wa vyombo vya habari kwa zaidi ya miaka 7.

Kazi yake[hariri | hariri chanzo]

Alifanya kazi na kampuni ya IPP Media, na baadae kupata uzoefu wa uhusiano wa umma na usimamizi wa matukio kwa takribani miaka 3.[1]Mnamo mwaka 2007, alikuwa mjumbe na meneja wa matukio ya kujitegemea.

Mnamo mwaka 2011, alizindua kampuni yake ya usimamizi wa matukio iitwayo Alta Vista Events. Kampuni hiyo inamiliki tamasha kubwa la Nyama Choma Afrika Mashariki na Kati. Kampuni hiyo pia inahimiza na kukuza ujasiriamali na kuingizwa kwa biashara ndogo hadi za kati na bidhaa zao mitaani zinazowapa wafanyabiashara kujulikana na kutoa fursa za ajira.

Carol alichaguliwa kwa Mpango wa Viongozi wa Vijana wa Afrika - Mfuko wa Maendeleo ya Mandela wa 2016.

Yeye ni mmoja wa waanzilishi wa suluhisho la kidigitali ambalo linaitwa KilimoUza, ambapo suluhisho hili linawapa fursa ya kuwaunganisha wakulima.

Carol pia ameanzisha Launch Pad Tanzania, ambayo inahusisha masuala ya kitaalamu ya maendeleo na kitovu cha maendeleo binafsi. Launch Pad inazingatia uwezeshaji wa vijana na wanawake kwa njia ya maendeleo ya ujuzi na mipango ya uwezeshaji wa kiuchumi.

Carol ni Championi wa Global Goals na Umoja wa Mataifa Tanzania. Alipigiwa kura na kuchaguliwa kama "Mwanamke wa Ushawishi" kwa Tuzo za Malkia Wa Nguvu 2018. Pia aliorodheshwa na Amazons kati ya viongozi 25 wa kike wanaojitokeza[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Caroline Ndosi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.