Nenda kwa yaliyomo

Candîce Hillebrand

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Candice Hillebrand
Amezaliwa Candice Hillebrand
19 Januari]] 1977
Johannesburg
Jina lingine Candîce
Kazi yake mtangazaji

Candice Hillebrand (pia anajulikana kama Candîce )amezaliwa katika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini, 19 Januari 1977) ni mwigizaji, mwimbaji na mwandishi wa nyimbo. Pia amefanya kazi kama mtangazaji na mwanamitindo.

Hivi karibuni anajulikana kwa kucheza filamu kama Nina Williams mwaka 2009 kwenye filamu za vitendo, alijiusha zaidi na mfululizo maarufu wa mchezo wa video Tekken.

Wasifu wa Hillebrand kwenye skrini ulianza mapema maishani mwake kwa kutangaza chaneli ya televisheni ya watoto ya Afrika Kusini, KTV, akiwa na miaka 6. Hillebrand aliendelea kuonekana katika matangazo mengi na pia aliigiza kwenye runinga na kwenye filamu. Mwaka 2002, alisaini na lebo ya Musketeer Records na kuachia albamu yake ya kwanza, Chasing Your Tomorrows mwaka 2003. Pia alionekana kwenye gazeti la Maxim.

Mwaka 2008, Hillebrand alipewa nafasi ya Nina Williams, mhusika wa mfululizo maarufu wa mchezo wa video Tekken.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Candîce Hillebrand kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.