Bongo Bahati Mbaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Bongo Bahati Mbaya”
“Bongo Bahati Mbaya” cover
Kava ya Bongo Bahati Mbaya
Single ya Young Dee
Imetolewa 5 Mei, 2017
Muundo Upakuzi wa mtandaoni[1]
Imerekodiwa 2017
Aina Hip hop, ragga dancehall
Urefu 3:53
Studio King Cash
Mtunzi Young Dee
Mtayarishaji Mr. T. Touch
Mwenendo wa single za Young Dee
"Bongo Bahati Mbaya"
(2017)
"Kiutani Utani"
2017

"Bongo Bahati Mbaya" (vilevile BBM) ni jina la wimbo uliotoka 5 Mei, 2017 wa msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania - Young Dee. Wimbo umetayarishwa na Mr. T. Touch. Huu ndio wimbo ambao huhesabiwa kama ujio mpya wa Young Dee. Kaboresha zaidi staili ya uimbaji na kadhalika. Ameongeza umakini na kufanya muziki kazi na si mizaha kama awali. Mnamo tarehe 28 Februari 2018, BASATA kupitia TCRA ilifungia wimbo huu pamoja na nyengine 14 zisipigwe katika vyombo vya habari nchini Tanzania kwa sababu zilizoelezwa ya kwamba zimekosa maadili.[2] Hata hivyo, Young Dee ameonekana kutosikitishwa na jambo hili hata kidogo. Hasa kwa madai ya kwamba hajapewa taarifa mapema wala fursa ya kujitetea.

Baadhi ya nyimbo zilizofungiwa na TCRA[hariri | hariri chanzo]

Nyimbo hizo ni pamoja na[3];

  1. Hallelujah - Diamond Platnumz
  2. Waka Waka - Diamond Platnumz
  3. Kibamia - ROSTAM, Roma na Stamina
  4. Pale Kati Patamu - Nay wa Mitego
  5. Hainaga Ushemeji - Man Fongo
  6. I am Sorry JK - Nikki Mbishi
  7. Chura - Snura Mushi
  8. Tema Mate Tumchape - Madee
  9. Uzuri Wako - Jux
  10. Nampa Papa - Gigy Money
  11. Nampaga - Barnaba Boy
  12. Maku Makuzi - Nay wa Mitego
  13. Nimevurugwa - Snura Mushi
  14. Bongo Bahati Mbaya - Young Dee
  15. Mikono Juu - Nay wa Mitego

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. BBM katika wavuti ya DJ Mwanga
  2. TRCA Yafungia Nyimbo za Diamond, Nay wa Mitego, Roma, Young Dee na Wengine Kisaa Hichi Hapa katika wavuti ya Udaka-Special.
  3. TCRA yafungia nyimbo 15 za bongo fleva Diamond,Jux,Roma,Nay wa mitego wamo. Archived 28 Februari 2018 at the Wayback Machine. katika wavuti ya Tabelltz. Ingizo la February 28, 2018.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]