Kichanganyi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Blender)
Kichanganyi cha jikoni.

Kichanganyi (kwa Kiingereza blender, mixer) ni kifaa kinachotumika jikoni katika kuchanganya na kusaga chakula kama vile matunda, chakula cha mtoto kilicho laini, smoothie na pia mboga. Kichanganyi hutumia kichuma kikali ambacho huzungushwa kwa kawaida na nguvu ya umeme kusaga na kuchanganya chakula. Kuna vichanganyi vyenye nguvu nyingi na kichuma kigumu hivi hata kuweza kusaga chakula kigumu kama mchele.

Sifa za kichanganyi[hariri | hariri chanzo]

Sifa ambazo watu huangazia wanapochagua kichanganyi kwa matumizi ya nyumbani ni kama vile:

  • Nguvu ambazo kichanganyi kinatumia kwa kawaida huwa kutoka wati 300 hadi 1000.
  • Urahisi wa kukisafisha.
  • Kelele zisizo nyingi wakati kinapofanya kazi.
  • Urahisi wa kukitumia.

Matumizi ya kawaida ya kichanganyi[hariri | hariri chanzo]

Kuchanganya aiskrimu, maziwa na michuzi yenye sukari katika kutengeneza milk shake

Kusaga mawe ya barafu na kuchanganya katika vinywaji vyenye pombe au hata visivyonayo.

Kutengeneza chakula laini cha mtoto kinachoitwa puree kwa kusaga vipande vikubwa ili viwe vidogo.

Kutengeneza viungo vya chakula kwa kuchanganya viungo vingi pamoja.

Historia ya kichanganyi[hariri | hariri chanzo]

Stephen J. Poplawski alianza pale Marekani kutengeneza kichanganyi cha vinywaji mwaka 1919 alipokuwa akifanya kazi na Arnold Electric Company. Muundo wake uliweza kuidhinishwa na kupewa patent mwakani 1922.

Mwaka 1930 Fred Osius aliweza kuboresha muundo wa Poplawski na kwa usaidizi wa mwimbaji Fred Waring, waliweza kukiuza kichanganyi baada ya kukibandika jina 'Miracle Mixer'.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]