Uzazi
Uzazi ni mchakato wa kibiolojia ambao kiumbe hai kipya kinapatikana kutokana na kingine au vingine.
Uwezo wa kuzaa ni kati ya sifa kuu zinazotambulisha uwepo wa uhai; kila kiumbe hai kilichopo duniani kimetokana na uzazi. Inakadiriwa kwamba kiumbe hai kilichozaa vile vyote vilivyopo leo kiliishi miaka 3,500,000,000 hivi iliyopita.
Njia za uzazi
[hariri | hariri chanzo]Kuna njia mbili za uzazi: ile isiyotegemea jinsia, na ile inayoitegemea.
Katika uzazi usiotegemea jinsia, kiumbe hai huzaa peke yake. Unatokea hasa katika viumbe vinavyoundwa na seli moja tu, lakini si hivyo tu. Kwa njia hiyo kiumbe hai kipya ni sawa na mzazi kwa sababu kimerithi jenomu ileile.
Wanabiolojia hawajaelewa ilikuwaje kwamba katika maendeleo ya uhai (mageuko ya spishi) uzazi huo umeacha nafasi kwa ule wa kijinsia unaodai wahusika wawe wawili, na hivyo kupunguza uzazi kwa asilimia 50.[1][2]
Uzazi wa kijinsia huwa unadai mchango wa wazazi wawili ambao kila mmojawao anakichangia kiumbe hai kipya kwa asilimia 50 za chembeuzi zake.
Uzazi wa binadamu
[hariri | hariri chanzo]Binadamu akiwemo kati ya mamalia anazaa kwa namna inayofanana hasa na ile ya wanyama hao. Hata hivyo, akiwa na akili na utashi, anatakiwa kuratibu silika yake kuhusu uzazi ili uendane na uwajibikaji.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Ridley M (2004) Evolution, 3rd edition. Blackwell Publishing, p. 314.
- ↑ John Maynard Smith The Evolution of Sex 1978.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Tobler, M. & Schlupp,I. (2005) Parasites in sexual and asexual mollies (Poecilia, Poeciliidae, Teleostei): a case for the Red Queen? Biol. Lett. 1 (2): 166-168.
- Zimmer, Carl. Parasite Rex: Inside the Bizarre World of Nature's Most Dangerous Creatures, New York: Touchstone, 2001.
- "Allogamy, cross-fertilization, cross-pollination, hybridization". GardenWeb Glossary of Botanical Terms (2.1 ed.). 2002.
- "Allogamy". Stedman's Online Medical Dictionary (27 ed.). 2004.
Marejeo mengine
[hariri | hariri chanzo]- Judson, Olivia (2003) Dr.Tatiana's Sex Advice to All Creation: Definitive Guide to the Evolutionary Biology of Sex. ISBN 978-0-09-928375-1
- The Evolution of Sex: An Examination of Current Ideas Richard E. Michod and Bruce E. Levin, editors (1987) Sinauer Associates Inc., Publishers, Sunderland, Massachusetts ISBN 0878934596 ISBN 978-0878934591
- Michod, R.E. Eros and Evolution: A natural philosophy of sex (1994). Addison-Wesley Publishing Company, Reading, Massachusetts ISBN 0201442329 ISBN 978-0201442328
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Asexual Reproduction Ilihifadhiwa 22 Januari 2018 kwenye Wayback Machine.
- Journal of Biology of Reproduction
- Journal of Andrology Ilihifadhiwa 7 Novemba 2005 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uzazi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |