Nenda kwa yaliyomo

Bet365 Stadium

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bet365 stadium)
Uwanja Wa Bet365

Bet365 Stadium ni uwanja wa mpira wa miguu huko Stoke-on-Trent, Staffordshire, Uingereza na nyumbani kwa klabu ya Stoke City F.C..

Uwanja wa Klabu hiyo ulikuwa unaitwa uwanja wa Britannia lakini ulibadilishwa jina tarehe 1 Juni 2016 wakati klabu iliingia mkataba mpya wa haki na jina la uwanja na kampuni yake, bet365.Uwanja una uwezo wa 30,089 baada ya kukamilika kwa kazi za upanuzi mwaka 2017.

Uwanja ulijengwa mwaka 1997 kwa gharama ya Paundi 14.7 milioni kama nafasi ya Uwanja wa Victoria. Mchezaji wa zamani Sir Stanley Matthews majivu yake yalizikwa chini ya Duara la kati kufuatia kifo chake Februari 2000; alifungua rasmi uwanja huo tarehe 30 Agosti,1997.Katika mashindano ya Ulaya unajulikana kama uwanja wa Stoke kutokana na kanuni za UEFA juu ya udhamini.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Bet365 Stadium kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.