Bendera ya Venezuela
Mandhari
Bendera ya Venezuela imepatikana tangu 12 Machi 2006 yenye nyota nane. Miaka ya nyuma ilikuwa na nyota saba tu. Nyota ya nane iliongezwa kwa heshima ya Simon Bolivar aliyekuwa kiogozi wa mapambano ya uhuru dhidi ya Hispania katika karne ya 19.
Bendera ina milia mitatu ya kulala ya njano, buluu na nyekundu.
Rangi hizi tatu zilikuwa bendera ya Francisco de Miranda aliyekuwa mtangulizi wa Simon Bolivar kama mwanamapinduzi wa Amerika ya Kusini dhidi ya ukoloni wa Hispania. Bendera yake ilionekana mara ya kwanza katika Venezuela mwaka 1806.
Rangi hizi zinatumiwa na bendera za nchi tatu za Kolombia, Venezuela na Ekuador ambazo zote tatu zilikuwa sehemu ya jamhuri ya kwanza ya Kolombia ("Kolombia kubwa") hadi mwaka 1831.