Bachir Belloumi
Mohamed El Bachir Belloumi (alizaliwa 1 Juni 2002) ni mchezaji wa soka wa Algeria katika klabu ya Kireno ya Farense, Belloumi, ni mtoto mdogo wa Lakhdar Belloumi, ambaye ni bingwa wa soka huko Algeria .
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Bachir Belloumi alianza kazi yake akiwa kijana na klabu ya GC Mascara. Baada ya hapo Tarehe 25 Agosti 2020, alihamishiwa kwenda katika klabu ya MC Oran. Tarehe 16 Januari 2021, Bachir Belloumi alipandishwa kwenye kikosi cha kwanza cha MC Oran, na akacheza mechi ya kwanza dhidi ya CR Belouizdad akiwa kama mchezaji wa akiba anaekaa benchi. Bao lake la kwanza katika soka lilikuwa dhidi ya US Biskra katika ushindi wa mabao 6-0, ambapo baba yake alikuwa ni moja ya shabiki aliyekuwa jukwaani akisherehekea ubingwa huo.Baada ya hapo Bachir Belloumi,Aliacha klabu hiyo na kwenda Ulaya mwezi Septemba 2021.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mercato : Belloumi résilie son contrat avec le MC Oran". dzfoot.com. 20 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2021.