Aïssa Khelladi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Aïssa Khelladi ni raia kutokea nchini Algeria, ni mwandishi wa habari, riwaya na maigizo, ambaye alichapisha vitabu vya misingi ya Kiislamu, tamthilia na riwaya mbalimabali ikiwemo Peurs et Mensonges na Rose d'abime. Riwaya hizi zote mbili zinajikita katika hali ya sasa ya Algeria.[1][2]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Aïssa Khelladi alizaliwa nchini Algeria mwaka1953, kabla ya vita vya Algeria ya kupambania uhuru wake kati ya chama cha ukombozi cha National Liberation Front (F.L.N) ya Algeria na serikali ya Ufaransa. Alianza kuhudhuria masomo ya Kurani katika umri mdogo kabla ya kujiunga na shule ya msingi na Sekondari huko Algiers kabla ya kuachana na masuala ya elimu pale ambapo si ya ulazima na kuisaidia familia yake. Alifanya mtihani wa baccalaureate kabla ya kuendelea na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Algiers na kutunikiwa shahada ya kwanza ya sanaa na DEA ambayo ni sawa na shahada ya uzamili ya saikolojia baada ya kupata mkopo kutoka wizara ya ulinzi ya Algeria. Baada ya kupata shahada ya kwanza, aliandika vitabu viwili kati ya mwaka 1981 na 1984, “Attende et Journal” na hadithi fupi.[3]

Mwaka 1988, aliachana na jeshi baada ya kufikia cheo cha ukapteni na kuhamishia mitazamo yake katika uandishi. Kujitolea kwake katika uandishi wa habari na riwaya ilichangia kuundwa na kuanzishwa kwa habari za Hebdo mnamo mwaka 1990. Baada ya hapo, alichapisha insha iitwayo “Les Islamistes Algeriens Face Au Pouvoir” ( Waislamu wa Algeria katika mamlaka), akichimbua ajenda za kidini za F.L.N na F.I.S. Insha hiyo ilipigwa marufuku na serikali ya Algeria na Khelladi alikimbia nchi baada ya majaribio ya kuuawa kwake kushindwa. Alipatiwa uhifadhi wa kisiasa na Ufaransa ambapo aliendelea na kazi yake. Akiwa Ufaransa, alichapisha riwaya nyingine iitwayo “Peurs et Mensonges” (“Fears and Lies”) mnamo mwaka 1996. Ndani ya mwaka huo, Khelladi alianzisha jarida la Algérie Littérature/Action akiwa pamoja na Marie Virolle. Ilhali akiwa bado Ufaransa, alichapisha riwaya mbili mwaka 1998, Rose d’Abime” na “Spolaition”.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Aïssa KHELLADI Africultures.com
  2. Toler, Michael; Aïssa Khelladi; Marie Virolle (July 2006). "Literature, Art, and a Country in Crisis". World Literature Today 80 (4): 16–20. JSTOR 40159128. doi:10.2307/40159128.  Check date values in: |date= (help)
  3. Khelladi, Aïssa, 1953- (1997). Peurs et mensonges : roman. Paris: Seuil. ISBN 2020312328. OCLC 37244769. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aïssa Khelladi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.