Augustine Lotodo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Augustine Chemonges Loile Lotodo ni Mkenya ambaye aligombea nafasi ya Naibu Rais katika uchaguzi wa Rais wa Kenya uliofanyika Machi 2013 kwa tiketi ya NARC-Kenya, kama mgombea mwenza wa Martha Karua.[1]

Lotodo alisoma Uchumi huko Rani Durgavati Vishwavidyalaya nchini India na ni mtoto wa Waziri wa zamani wa Baraza la Mawaziri Francis Lotodo. Mnamo 2002, aligombea kiti cha ubunge cha Jimbo la Kapenguria bila mafanikio. Kati ya 2004-2006, alikuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maji ya Ziwa Victoria Kaskazini iliyoko Kakamega. Alikuwa mwanachama wa Bunge la Afrika Mashariki lililoko Arusha, Tanzania kati ya 2007-2012.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "House committee clears shuttle for AMS flight". Physics Today. 2008. ISSN 1945-0699. doi:10.1063/pt.5.022287. 
  2. "Running Mate", Elections A to Z (CQ Press), ISBN 978-0-87289-366-5, iliwekwa mnamo 2021-06-29 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Augustine Lotodo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.