Punda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Asinus)
Punda
Punda-kaya katika Hifadhi ya Taifa ya Amboseli
Punda-kaya katika Hifadhi ya Taifa ya Amboseli
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Perissodactyla (Wanyama wenye kidole kimoja au vitatu miguuni)
Familia: Equidae (Wanyama walio na mnasaba na farasi)
Jenasi: Equus (Farasi na punda)
Linnaeus, 1758
Nusujenasi: Asinus
Ngazi za chini

Spishi 3, nususpishi 12:

Punda ni wanyama wakubwa kiasi wa nusujenasi Asinus ya jenasi Equus katika familia Equidae wafananao na farasi mdogo. Spishi moja (Equus kiang), ambayo inatokea Asia, huitwa kiang'. Punda anayejulikana sana ni yule anayefugwa (Punda-kaya), lakini kuna punda porini pia. Watu huwatumia punda wafugwao kwa kubeba mizigo, kuvuta magari au kuwarakibu. Punda wanaweza kuzaliana na farasi lakini watoto wao (baghala au nyumbu) hawazai tena kwa kawaida.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Crystal Clear app babelfish vector.svg Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Punda kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.