Nenda kwa yaliyomo

Asidi ya asetiki (matumizi ya kimatibabu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Asidi ya asetiki
Fomyula ya kemikali ya asidi asetiki
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Acetasol, Vasotate, Acid Jelly, Domeboro Otic, mengineyo
AHFS/Drugs.com Monograph
Taarifa za leseni US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito ?
Hali ya kisheria -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Matone ya sikio
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe Siki
Data ya kikemikali
Fomyula C2H4O2
Massi ya molekuli 60.052

Asidi ya asetiki, ambayo ikiwa katika viwango vya chini hujulikana kama siki, ni asidi inayotumiwa kutibu magonjwa kadhaa. Kama dawa ya matone ya sikio hutumika kutibu maambukizi ya mfereji wa sikio.[1] Inaweza kutumika kwa utambi wa sikio.[2] Kama kimiminika, hutumika kusafisha kibofu cha mkojo kwa wale walio na mpira wa mkojo ili kuzuia maambukizi au kuziba.[3] Kama jeli, inaweza kutumika kurekebisha pH ya uke.[4] Inaweza pia kutumika kwa seviksi ili kusaidia kugundua saratani ya shingo ya kizazi wakati wa uchunguzi.[5]

Madhara yake yanaweza kujumuisha kuchoma kwenye eneo la ambapo imepakwa.[6] Athari za mzio zinaweza kutokea mara chache.[6] Haipendekezwi kutumia katika sikio kwa watu ambao wana shimo kwenye kiwambo cha sikio.[7] Inafanya kazi dhidi ya sababu zote za bakteria na kuvu za maambukizo ya sikio la nje.[7]

Asidi ya asetiki imekuwa ikitumika kimatibabu tangu wakati wa Misri ya Kale.[8][9] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[10] Asidi ya asetiki inapatikana kama dawa ya kawaida. [2] Nchini Marekani, kozi ya matibabu na utayarishaji wa sikio inagharimu chini ya $25.[2] Asidi ya asetiki hutumiwa zaidi kwa maambukizi ya sikio la nje katika nchi zinazoendelea kuliko zilizoendelea.[11]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Acetic acid (otic) medical facts from Drugs.com". www.drugs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 Hamilton, Richart (2015). Tarascon Pocket Pharmacopoeia 2015 Deluxe Lab-Coat Edition. Jones & Bartlett Learning. uk. 252. ISBN 9781284057560.
  3. "Acetic Acid". The American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Acetic acid gel: Indications, Side Effects, Warnings - Drugs.com". www.drugs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Fokom-Domgue, J; Combescure, C; Fokom-Defo, V; Tebeu, PM; Vassilakos, P; Kengne, AP; Petignat, P (3 Julai 2015). "Performance of alternative strategies for primary cervical cancer screening in sub-Saharan Africa: systematic review and meta-analysis of diagnostic test accuracy studies". BMJ (Clinical research ed.). 351: h3084. doi:10.1136/bmj.h3084. PMC 4490835. PMID 26142020.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 "Acetic acid otic Side Effects in Detail - Drugs.com". www.drugs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 "Acetic Acid - FDA prescribing information, side effects and uses". www.drugs.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 14 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Cook, Larry (2005). The Beginner's Guide to Natural Living: How to Cultivate a More Natural Lifestyle to Lose Weight, Prevent Degenerative Disease, Improve Your Energy and Attain Vibrant Health (kwa Kiingereza). EcoVision Communications. uk. 107. ISBN 9780975536186. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-16.
  9. Cumston, C. G. (2013). The History of Medicine (kwa Kiingereza). Routledge. uk. Chapter 2. ISBN 9781136194252. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-16.
  10. World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.{{cite book}}: CS1 maint: location missing publisher (link)
  11. Desai, Bobby; Desai, Alpa (2016). Primary Care for Emergency Physicians (kwa Kiingereza). Springer. uk. 36. ISBN 9783319443607. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-16.