Arthur Rimbaud
Jean Nicolas Arthur Rimbaud (20 Oktoba 1854 - 10 Novemba 1891) alikuwa mshairi kutoka nchini Ufaransa. Alizaliwa kama mtoto wa mwanjeshi huko Charleville katika kaskazini-mashariki ya Ufaransa. Wakati wa vita ya Ujerumani dhidi ya Ufaransa ya 1870/71 alijitolea kuwa mwanajeshi akiwa na umri mdogo wa miaka 16 tu. Wakati uke aklianza kuandika mashairi yaliyohusu mwanzoni alichoona vitani.
Wakati ule alijitambua kuwa alivutiwa na jinsia ya kiume aka na uhusiano wa kipenzi na mshairi Paul Verlaine mkubwa wake.
Kati ya 1873 hadi 1873 alitoa vitabu 2 vya mashairi lakini alipofikia miaka 21 aliacha kuandika akaanza kuzunguka duniani. Alikaa miaka mingi Afrika ya Kaskazini na kwenye nchi kando la Bahari ya Shamu kama vile Yemen na Uhabeshi. Alifanya biashara ya kahawa, dhahabu, meno ya tembo na silaha. Kwa muda wa miaka saba alikaa mjini Harar alipokuwa rafiki wa gavana Ras Makonnen baba waHaile Selassie aliyekuwa baadaye Negus wa Uhabeshi.
1891 aligonjeka goti akaona vema kurudi Ufaransa kwa tiba; mguu wake ulikatwa na madaktari lakini sababu ya ugonjwa ilikuwa kansa ya mfupa akafa tar. 10 Novemba 1891 mjini Marseille akiwa na umri wa miaka 37.