Kisukari (samaki)
Mandhari
(Elekezwa kutoka Ariommatidae)
Kisukari | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kisukari fedha (Ariomma bondi)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 7, 2 katika Afrika ya Mashariki:
|
Visukari au haluwa ni samaki wadogo hadi wastani wa baharini wa jenasi Ariomma, jenasi pekee ya familia Ariommatidae katika oda Perciformes, wanaotokea maji ya kina kikubwa.
Pezimgongo la visukari limegawanyika katika mapezi mawili. Lile la mbele lina miiba 10-12 na lile la nyuma lina tindi 14-18. Kuna mikuku minono miwili kila upande wa msingi wa mkia. Urefu wao ni sm 20-35 na kipeo cha sm 80 (kisukari mapezi-mafupi).
Hula gegereka wadogo na planktoni wanyama.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Ariomma bondi, Kisukari Fedha (Silver-rag driftfish)
- Ariomma brevimanum, Kisukari Mapezi-mafupi (Shortfin driftfish)
- Ariomma indicum, Kisukari Hindi (Indian driftfish)
- Ariomma melanum, Kisukari Mweusi (Brown driftfish)
- Ariomma parini, Kisukari wa Parin (Parin's ariomma)
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Ariomma luridum (Ariommid)
- Ariomma regulus (Spotted driftfish)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kisukari hindi pamoja na mchanga
-
Kisukari mweusi
-
Spotted driftfish
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Visukari kwenye hifadhidata ya samaki Ilihifadhiwa 8 Desemba 2022 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kisukari (samaki) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |