Aneesa Ahmed

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Aneesa Ahmed
Aneesa Ahmed alipokea Tuzo ya Kimataifa ya Wanawake wa Ujasiri kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton na Mama wa Kwanza Michelle Obama mwaka 2012.


Aneesa Ahmed ni mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka mchi ya Maldivi ambaye pia alikuwa Spika wa kwanza (naibu) wa Majilis toka 2004 hadi 2009.[1]

Alisoma kama Mshirika wa Humphrey katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania kuanzia mwaka 1985 hadi 1986[2]. Baadaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Wanawake huko Maldivi, ambapo alileta mada ya ukatili wa ndani licha ya kwamba ilikuwa ni jambo la kuchukiza kufanya hivyo. Baada ya kutumikia serikalini, alianzisha shirika lisilo la kiserikali ("Hope for Women") na kuongoza vikao kuhusu ukatili wa kijinsia na polisi, wanafunzi, na wengine[3]. Wakati redio ya kitaifa ya Maldives ilipoanza kuonyesha wasomi wa kidini ambao walidai ukeketaji wa wanawake uliungwa mkono na Uislamu, aliiomba serikali kuingilia kati, na kuzungumzia kwa uwazi juu ya madhara ya ukeketaji wa wanawake.

Alitunukiwa tuzo [4]ya Wanawake wa Kimataifa wa Ujasiri ya mwaka 2012. Alikuwa mwanamke wa pili kutoka Maldivi kupokea Tuzo ya Wanawake wa Kimataifa wa Ujasiri.[5]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aneesa Ahmed kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.