Nenda kwa yaliyomo

Majarra ya Mara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Andromeda (galaksi))
Majarra ya Mara (Andromeda Galaxy)
Galaksi ya Andromeda
Kundinyota Mara (Andromeda)
Mwangaza unaonekana +3.44
Umbali (miakanuru) milioni 2.5
Mwangaza halisi -21.5
Masi M☉ 1.5×1012
Majina mbadala Messier 31, M31, NGC 224


Majarra ya Mara (ing. Andromeda Galaxy, inajulikana pia kama Messier 31, M31 au NGC 224) ni majarra kubwa iliyo karibu zaidi na majarra yetu ya Njia Nyeupe. Umbali wake na Dunia ni takriban miakanuru milioni 2.5. Inaonekana katika eneo la kundinyota la Mara linaloitwa "Andromeda" kwa jina la kimataifa na hii ni chanzo cha jina lake. Ni sehemu ya kundi janibu la majarra pamoja na Njia Nyeupe, Mawingu ya Magellan na takriban majarra 40 nyingine.

Ina mwangaza unaoonekana wa mag 3.4 na hivyo inaonekana kama nyota hafifu kwa mtazamaji. Hivyo ni kiolwa cha anga cha mbali kinachoonekana bila darubini.

Tabia

Umbali wa majarra ya Mara hadi mfumo wa Jua letu ni takriban miakanuru milioni 2.5. Kipenyo chake cha jumla (pamoja na fungunyota za nje) ni takriban miakanuru milioni moja. Masi yake imekadiriwa kuwa mnamo masi za Jua 1.5×1012 au mara trilioni 1.5 ya masi ya Jua letu. Hivyo ni kubwa kuliko Njia Nyeupe iliyokadiriwa kuwa na M☉ 8×1011.

Kipenyo cha diski inayoonekana hukadiriwa kuwa miakanuru 140,000 hadi 220,000.


Marejeo

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Majarra ya Mara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.