Nenda kwa yaliyomo

Amur

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Amur River)
Amur
Mto Amur karibu na Heihe (China) ikitazama Urusi
Mto Amur karibu na Heihe (China) ikitazama Urusi
Chanzo Milima ya Khingan katika Mongolia ya Kichina.
Mdomo Bahari ya Ohotsk
Nchi za beseni ya mto Urusi, China
Urefu 2,824 km
4,666 km pamoja na mto Argun
Kimo cha chanzo 800 m
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni 11,000 m³/s
Eneo la beseni (km²) 1,929,955 km²
Beseni la Amur.

Amur (kwa Kirusi: Амур; kwa Kichina: heilong jiang) ni mto mkubwa wa Asia ya Mashariki ambao ni mpaka kati ya Urusi na China kwa maelfu ya kilomita.

Amur ina chanzo chake penye kuungana kwa matawimto ya mto Argun na mto Shilka karibu na kijiji cha Moguhe katika jimbo la Heilongjiang. Kuanzia hapo inafuata mwendo wake kwa urefu wa 2,874 km hadi kuishia katika Bahari ya Ohotsk (Pasifiki) karibu na kisiwa kikubwa cha Sakhalin. Matawimto Argun na Shilka yanaanza katika Mongolia yenyewe na Mongolia ya Kichina.

Pamoja na mwendo wa Argun urefu wa mto wote ni takriban km 4,666, hivyo ni mto mrefu wa nane duniani.

Amur imekuwa mpaka kati ya China na Urusi tangu mkataba kati ya nchi hizi wa tarehe 27 Agosti 1689.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Amur kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.