Amur

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Amur (mto))
Jump to navigation Jump to search
Amur
Mto Amur karibu na Heihe (China) ikitazama Urusi
Mto Amur karibu na Heihe (China) ikitazama Urusi
Chanzo Milima ya Khingan katika Mongolia ya Kichina.
Mdomo Bahari ya Ohotsk
Nchi za beseni ya mto Urusi, China
Urefu 2,824 km
4,666 km pamoja na mto Argun
Kimo cha chanzo 800 m
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni 11,000 m³/s
Eneo la beseni (km²) 1,929,955 km²
Beseni ya Amur

Amur (Kirusi: Амур; Kichina: heilong jiang) ni mto mkubwa wa Asia ya Mashariki ambao ni mpaka kati ya Urusi na China kwa maelfu ya kilomita.

Amur ina chanzo chake penye kuungana kwa tawimito ya Argun na Shilka karibu na kijiji cha Moguhe katika jimbo la Heilongjiang. Kuanzia hapa inafuata mwendo wake kwa urefu wa 2,874 km hadi kuishia katika Bahari ya Ohotsk (Pasifiki) karibu na kisiwa kikubwa cha Sakhalin. Tawimito Argun na Shilka inaanza katika Mongolia yenyewe na Mongolia ya Kichina.

Pamoja na mwendo wa Argun urefu wa mto wote ni takriban 4,666 km hivyo mto mrefu wa nane duniani.

Amur imekuwa mpaka kati ya China na Urusi tangu mkataba kati ya nchi hizi wa tar. 27 Agosti 1689.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]