Nenda kwa yaliyomo

Almoravid Qubba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Almoravid Qubba (kwa Kiarabu: القبة المرابطية) au Qubba Ba'adiyyin / Barudiyyin, ni ukumbusho mdogo huko Marrakech, nchini Moroko. Ulijengwa na nasaba ya Almoravid mwanzoni mwa karne ya 12.[1] Unajulikana kwa mapambo yake ya ajabu na kuwa moja ya mabaki tu ya usanifu wa Almoravid huko Marrakech.[2]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jengo la Almoravid Qubba lipo karibu na jumba la makumbusho ya Marrakech karibu mita 40 kusini mwa msikiti wa Ben Youssef. Ni mfano pekee uliobaki wa usanifu wa Almoravid huko Marrakech. Ulijengwa na Almoravid Amir Ali ibn Yusuf mnamo mwaka 1117 au mnamo mwaka 1125.[3][4] Wasomi wengi leo wanaamini kuwa ulimilikiwa na msikiti wa karibu wa Ben Youssef, msikiti mkuu wa jiji kwa wakati huo, na kwamba ulikuwa sehemu iliotumiwa kwa ajili ya kutawadha kabla ya sala.[3][2][5] Msikiti wenyewe ambao ulijengwa awali na Ali ibn Yusuf tangu wakati huo, umekamilika kujengwa kabisa katika karne za hivi karibuni.[2]. Aina hii ya mfumo wa ugawaji wa maji karibu na msikiti ilijulikana kama mida'a na hupatikana pia katika misikiti ya baadaye huko Marrakech.[4]

Uwepo wa Qubba uliandikwa kwanza na wasomi wa Ufaransa mnamo 1947 na msanifu wa kihistoria Boris Maslow akichapisha maelezo mnamo mwaka 1948. Kwenye miaka inayofuata kwa undani zaidi, uchunguzi na tafiti zilifanywa chini ya uongozi wa Henri Terrasse na Jacques Meunie. Kwa sababu ya kiwango cha chini cha ardhi na ujenzi wa miundo mingine inayoizunguka, zaidi ya nusu ya Qubba ilifukiwa chini mita 7-8 ya uchafu. Wasomi wa Ufaransa walijizuia kufanya ujenzi wowote muhimu au urejesho wakiacha muundo kimsingi kama ulivyopatikana na kuchapisha matokeo yao miaka ya 1950. Kwenye karne toka ulivyogundulika umekuwa ndio ukumbusho wa kihistoria na kivutio cha watalii.[6][7]

Ukumbi huo wa (qubba) uko juu ya jengo la mstatili, lenye urefu wa mita 7.35 na 5.45, na kuhifadhi bonde la maji. Muundo wote una urefu wa mita 12. Vifaa vilivyotumika ni pamoja na mawe, matofali na mbao za mwerezi. Ndani pamepambwa sana na maua ya kuchonga na muundo wa mboga (mbegu za misonobari, mitende na majani ya acanthus), maumbo ya mitende, koa za baharini, na kaligrafia.

  1. الإسبانية, دورية قنطرة. "حول القبة المرابطية في مراكش". المراكشية : بوابة مراكش (kwa Kiarabu). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-31. Iliwekwa mnamo 2020-05-19. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 Deverdun, Gaston (1959). Marrakech: Des origines à 1912. Rabat: Éditions Techniques Nord-Africaines.
  3. 3.0 3.1 Bennison, Amira K. (2016). The Almoravid and Almohad Empires. Edinburgh University Press. ku. 309–10, 322–25.
  4. 4.0 4.1 Salmon, Xavier (2018). Maroc Almoravide et Almohade: Architecture et décors au temps des conquérants, 1055-1269. Paris: LienArt.
  5. Marçais, Georges (1954). L'architecture musulmane d'Occident. Paris: Arts et métiers graphiques. uk. 200.
  6. Parker, Richard (1981). A practical guide to Islamic Monuments in Morocco. Charlottesville, VA: The Baraka Press. ku. 58-59.
  7. "Almoravid Koubba | Marrakesh, Morocco Attractions". Lonely Planet (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-01-30.