Almasi za damu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtu akichuja almasi huko Sierra Leone.
Makala ya video inayoelezea uUchimbaji wa almasi usiyo-faa huko nchini Sierra Leone. (Kiingereza)

Almasi za damu (pia: almasi zenye mgogoro; kwa Kiingereza: Blood diamonds, conflict diamonds, war diamonds, hot diamonds, au red diamonds) ni istilahi inayotumiwa kwa ajili ya almasi zinazochimbwa katika ukanda wenye vita na kuuzwa na hatimaye kufadhili machafuko ya kivita katika ukanda husika. Istilahi hiyo inatumika kuangazia matokeo mabaya ya biashara ya almasi katika baadhi ya maeneo, au kupachika majina kwa wauzaji au muuzaji anayejihusisha na almasi zinazotokana na maeneo hayo.

Almasi zilizochimbwa hivi karibuni katika kanda za kivita huko nchini Angola, Ivory Coast, Sierra Leone, Liberia, Guinea, Ghana, na Guinea Bissau zote zimepewa jina la almasi za damu.[1][2][3] Hali hii ilikuja kupata ufumbuzi baada ya azimio la "Mkataba wa Kimberley".

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Conflict Diamonds. United Nations Department of Public Information, March 21, 2001, archived online 23 October 2013.
  2. "Conflict resources: from 'curse' to blessing" by Ernest Harsch. Africa Renewal: January 2007.
  3. "Global Summary 2008" (PDF). Kimberley Process Certification Scheme. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-26.