Alkoholi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Alkoholi (pia: alikoholi) ni jina kwa kundi la viowevu visivyo na rangi. Neno latumiwa mara nyingi kutaja aina yoyote ya pombe; hali halisi ni aina moja ya alkoholi ambayo ni alkoholi ethili iliyopo ndani ya aina zote za pombe na kusababisha ulevi.

Katika elimu ya kemia alkoholi ni kampaundi ogania yoyote yenye kundi hidroksidi (–O–H) iliyounganishwa na atomi ya kaboni.

Alkoholi zinatokea kiasili katika kampaundi nyingi. Ethili hutokea kiasili wakati wa kuchachuka kwa matunda au majimaji yenye sukari ikitengenezwa na bakteria.

Matumizi ya alkoholi inayojulikana hasa ni yale ya ethanoli katika vinywaji. Uchumi wa kisasa hutumia aina nyingi za alkoholi mbalimbali kama madawa katika utengezaji wa vitu. Alkohili zina matumizi kama fueli au madawa ya kuyeyusha na kusafisha. Madawa ya tiba hutengenezwa mara nyingi kwa kutumia alkoholi inayoyeyusha dutu katika mimea au mizizi inayotumika kwa kutibu watu.


Aina za alkoholi[hariri | hariri chanzo]

Alikoholi zinazotumiwa mara nyingi ni methanoli (au alkoholi methili) na ethanoli (au alkoholi ethili). Zina muundo ufuatao:

   H      H H
   |      | |
  H-C-O-H   H-C-C-O-H
   |      | |
   H      H H 
 methanoli  ethanoli