Nenda kwa yaliyomo

Ethanoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Alkoholi ethili)
Muundo wa kikemia wa ethanoli. C ni kaboni, H ni hidrojeni na O ni oksijeni.
Molekuli ya ethanoli (hidrojeni ni nyeupa, kaboni ni kijivu na oksijeni nyekundu)
A bottle of Ethanol

Ethanoli (pia: alkoholi ethili) ni dawa lililopo ndani ya aina zote za vinywaji vya pombe.

Kikemia ni kampaundi ogania inayopatikana kama kiowevu kisicho na rangi. Ikiwa ni dawa safi inawaka haraka lakini mara nyingi hupatikana kama mchanganyiko pamoja na maji katika aina za pombe; hapa inawaka tu kama asilimia yake inapita kiwago cha 60%.

Fomula yake ni C2H5OH inayoandikwa pia C2H6O. Ni dawa lenye tabia ya sumu kiasi kwa mwili wa kibinadamu pia ina tabia ya kuyeyusha.

Ethanoli kama fueli

[hariri | hariri chanzo]

Ethanoli ina pia matumzi ya fueli badala ya petroli. Inawaka ndani ya injini ama peke yake au ndani ya mchanganyiko wa petroli na ethanoli.

Nchini Brazil ethanoli hutengenezwa kwa wingi kutokana na miwa na sasa inatosheleza asilimia 18 ya mahitaji ya fueli ya magari katika nchi hii. [1] Watu wengine wanaona tatizo katika teknolojia hii maana mashamba makubwa yanatumiwa kwa miwa hayapatiokani tena kwa vyakula na maeneo makubwa ya misitu asilia yametumiwa pia..

  1. "America and Brazil Intersect on Ethanol". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-26. Iliwekwa mnamo 2010-08-22.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ethanoli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.