Ali Bongo Ondimba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ali Bongo Ondimba

Ali-Ben Bongo Ondimba (amezaliwa na jina la Alain Bernard Bongo mnamo tar. 9 Februari 1959[1]) ni mwanasiasa kutoka nchini Gabon ambaye kwa sasa ni Rais wa Gabon kwa kufuatia ushindi wake kwenye uchaguzi wa rais wa 2009.

Bongo i mtoto wa Omar Bongo, ambaye alikuwa Rais waGabon kuanzia mwaka wa 1967 hadi kifo chake mnamo 2009. Wakati wa uongozi wa urais wa baba yake, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kuanzia 1989 hadi 1991 na kuwakilisha Bongoville akiwa kama Naibu Katibu wa Baraza la Bunge kuanzia 1991 hadi 1999; baadaye akawa Waziri wa Ulinzi kuanzia 1999 hadi 2009.

Alikuwa Makamu wa Rais wa Gabonese Democratic Party (PDG)[2] na alikuwa mgombea wa PDG kwenye uchaguzi wa rais wa Agosti 2009, ambapo ilifuatia na kifo cha baba yake.[3] Kulingana na matokeo rasmi, ameshinda uchaguzi na kura za 42%.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "BONGO Ali", GABON: LES HOMMES DE POUVOIR N°4, Africa Intelligence, 5 Machi 2002 (Kifaransa).
  2. PDG Vice-Presidents, PDG website (Kifaransa).
  3. "Bongo's son to be Gabon candidate in August poll", AFP, 16 Julai 2009.
  4. "Unrest as dictator's son declared winner in Gabon", Associated Press, 3 Septemba 2009.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]