Alexander Graham Bell

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alexander Graham Bell

Alexander Graham Bell (3 Machi 18472 Agosti 1922) alikuwa kati ya wagunduzi wa mawasiliano ya simu. Alizaliwa katika mji wa Edinburgh nchini Uskoti lakini baadaye alihamia nchi za Kanada na Marekani. Baba yake alikuwa mwalimu wa watoto wenye matatizo ya kusikia na kuongea. Alifanikiwa katika jaribio lake la kwanza mwaka 1876.[1]

Bell hakuwa mtu wa kwanza wa kutengeneza simu kwa mawasiliano lakini mashine yake ilikuwa ya kwanza iliyoweza kutumiwa kibiashara nje ya majaribio na maabara. Alitumia matokeo ya utafiti wa watangulizi hasa Mwitalia Antonio Meucci.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Alexander Graham Bell Laboratory Notebook, 1875-1876". World Digital Library. 1875–1876. Iliwekwa mnamo 2013-07-23.{{cite web}}: CS1 maint: date format (link)