Aleksander Pushkin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aleksander Pushkin

Aleksander Sergeyevich Pushkin (Kirusi Александр Сергеевич Пушкин; *6 Juni 1799 mjini Moskva; † 10 Februari 1837 Sankt Petersburg) alikuwa mwandishi na mshairi nchini Urusi.

Amesifiwa kama mwandishi mkuu wa fasihi ya Kirusi. Alikuwa mwandishi wa kwanza aliyefaulu kuandika kwa Kirusi kilichoeleweka na wananchi badala ya kutumia lugha ya kale jinsi ilivyokuwa kawaida kanisani. Waandishi wote wa Kirusi waliomfuata waliathiriwa naye.

Babu yake Pushkin alikuwa Mwafrika Abram Petrovich Gannibal aliyewahi kufika Urusi kama mtoto mtumwa aliyenunuliwa na balozi Mrusi kutoka milki ya Osmani na kupewa kama zawadi kwa tsar Peter Mkuu aliyemlea na kumfanya mtumishi wa serikali kwenye ngazi ya juu.